PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amesema maelfu ya wananchi wanaojitokeza katika mikutano yake ya kampeni ni uthibitisho kuwa wameridhishwa na kazi inayofanywa na chama hicho.
Sambamba na hilo, amegusia wale wanaohoji kwa nini CCM inatumia nguvu ilhali upinzani haupo, akisema , “ukidharau mwiba mguu huota tende.”
Samia amesema hayo, leo Jumapili, Septemba 7, 2025, aliposimama na kuzungumza na wananchi wa Mtera mkoani Dodoma, ikiwa ni mwendeleo wa kampeni zake za urais.
“WanaCCM wameridhishwa na kazi nzuri iliyofanyika, ndiyo maana kila tunapokanyaga, hakuna umma kuna utitiri, watu ni wengi, Ni wengi kwa sababu wameridhishwa na kazi iliyofanywa na Chama cha Mapinduzi,” amesema.
“Wanajadili huko, kwa nini mama anatumia nguvu sana wakati upinzani haupo, waswahili wanasema anayedharau mwiba ukimchoma mguu unaota tende, sasa usisubiri mpaka uchomwe na msumari hapana, hata mwiba lazima uushughulikie,” amesema.