GE2025 Samia awajibu wanaodai CCM inatumia nguvu kubwa kwenye kampeni

GE2025 Samia awajibu wanaodai CCM inatumia nguvu kubwa kwenye kampeni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hii inamaanisha waziwazi kuwa upinzani madhubuti ungemuwa wa CHADEMA ya Lissu

Hawa akina Act Wazalendo ni kama vijimiba ambavyo hata vikikuchoma hauumii.

Ni dhahiri kuwa bila CHADEMA ya Lissu hakuna upinzani wa kweli.
Mkuu tupia video tusikilize
 
Hii inamaanisha waziwazi kuwa upinzani madhubuti ungemuwa wa CHADEMA ya Lissu

Hawa akina Act Wazalendo ni kama vijimiba ambavyo hata vikikuchoma hauumii.

Ni dhahiri kuwa bila CHADEMA ya Lissu hakuna upinzani wa kweli.
Oh nilikuwa sijamuelewa ila sasa nimeelewa kumbe alikuwa anamaanisha hivyo, asante kwa ufafanuzi mkuu.

Mwisho atasema yote aliyoyafanya mabaya
 
MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti waTaifa , Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema hawakidharau chamachochote kinachoshiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, mwakahuu.

Dkt. Samia ameyasema hayo Jumapili Septemba 7 wakati akizungumza naumati wa wananchi huko Mlowa katika Jimbo la Mvumi Wilaya yaChamwino mkoani Dodoma.

Amesema: "Wanajadili huko kwa nini CCM inatumia nguvu sana wakati upinzani haupo, waswahili wanasema ‘anayedharau mwiba ukimchoma mguu unaota tende, sasa usisubiri mpaka uchomwe na msumari. Hapana!Hata mwiba lazima uushughulikie". “Kama misumari imelala, hii miiba iliyochomoza na kusimama lazima tuishughulikie ipasavyo," amefafanua mgombea huyo wa urais kwa CCM.

Alisema pia wana CCM wameridhishwa na kazi nzuri iliyofanyika na ndio maana wamekuwa wakihudhuria kwa wingi mikutano ya kampeni.“Wana CCM wameridhishwa na kazi iliyofanywa na ndio maana kilatunapokanyaga kuna utitiri, watu ni wengi kwa sababu wameridhishwa naSerikali ya Chama Cha Mapinduzi na hilo ndio jawabu kubwa zaidi kulikoyote," alieleza Dkt. Samia.

Akijibu maombi ya mgombea ubunge wa jimbo hilo, Livingstone Lusinde lakuomba maji na barabara, Dkt. Samia alisema anayachukua na kwendakuyafanyia kazi.

Kuhusu ombi la kujengewa shule ya sekondari ya kuanzia kidato chakwanza hadi cha sita, amesema hilo anakwenda kulitekeleza na piaanatambua kuna kata tatu hazina kabisa sekondari nazo zitajengewa.

“Mimi kama mama, mtazamo wangu uko palepale, mama anataka watoto washibe kwanza ndiye yeye afuate, najua nina watoto wa kulea na ninajuawana masilahi yao lazima niyazingatie," aliongeza Dkt. Samia.

Akiwa kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa katika mkutano mkubwa wakampeni, amesema serikali yake imejipanga kufufua na kujenga ushirikaimara kwa ajili ya kuwainua wakulima na wanaushirika nchini.

Na katika hilo, amesema vyama hivyo vitabidi vijikite katika matumizi yaTeknolojia ya Habari na Mawasiliano ili kudhibiti ubadhirifu kupitia mapatona matumizi.

Amesema serikali yake inakusudia kufufua na kujenga ushirika imaraambao utaendesha mambo yake wenyewe ikiwamo kujipatia mikopo,kujenga maghala na kutafu kutafuta masoko.

"Kwa usimamizi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, vyama vya ushirikavijiendeshe vyenyewe na viwe na nguvu. Tunataka vyama vya ushirikavifaidi nguvu ya jasho lao na kumuinua mkulima," alieleza Dkt. Samia.

Amesema serikali itahakikisha vyama hivyo vinaendeshwna na watu mahirina vinatumia Tehama katika hesabu zake.Amewaahidi wafanyabiashara mjini Iringa kujenga Soko la Machinga, natayari eneo na fedha vipo.​
 

Attachments

Back
Top Bottom