ChoiceVariable anaamini ndio rais bora kuwahi kutokea Tanzania!
Nashawishika kuanzisha mada ya kuchambua makundi ya watu wanaomuunga mkono Samia.
Hawa watu, ni mambo yapi hasa yanafanya wagande na Samia hata akifanya mabaya kiasi gani?
Chukulia mtu kama Luca Mwashambwa, au Tlaatlaah, au Stuxnet; Steven Joel Ntamusana, stroke na wengi wengine, ni sifa zipi alizonazo Samia zinazowavuta wote hawa kwake?
Najuwa anazo sifa chache ambazo zipo wazi; kama dini yake, au uwezo wa kununua baadhi yao, au maslahi ya ajira/vyeo, n.k.
Wote hawa najuwa wanafiti katika kila kundi kati ya hayo niliyoyataja na mengineyo. Inaniwia vigumu kufikiri kuwa wapo ambao wanampenda na kumtetea Samia kwa sababu ya uwezo wake wa kuitumikia Tanzania na kulinda maslahi ya watu wake.
Kama wapo, itabidi nichambue maoni ya michango yao mbalimbali humu Jukwaani kuona uamini wao huo.