tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema dhamira ya serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha akina mama wanajifungua salama bila kupoteza maisha, akisisitiza kuwa kuleta maisha mapya isiwe sababu ya kifo cha mama mjamzito.
Akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Stendi ya Mabasi Same, mkoani Kilimanjaro leo Septemba 30, 2025, Dkt. Samia amesema uzoefu wake wa mwaka 2015 alipokuwa mgombea mwenza katika ziara ya kampeni Same, ndiyo uliozidisha dhamira yake ya kuimarisha huduma za afya nchini.
Soma pia: mtu anayefanya mauwaji sababu ya madaraka ni chizi viongozi wa dini wanapaswa kuimarisha ulinzi wao wakati huu pale wanapo hamasisha haki
“Mwaka 2015 nilipoanza kampeni kwa mara ya kwanza kituo cha kwanza kilikuwa Same. Nilienda kwenye zahanati moja pale Hedaru na hali ya huduma kwa wajawazito haikunifurahisha. Nikaweka nia ya kubadilisha hali hiyo kwa Tanzania nzima. Leo namshukuru Mungu, tumeimarisha huduma na tutaendelea kujenga hospitali za wilaya, vituo vya afya na zahanati zenye vifaa kamili,” amesema Dkt. Samia.
Ameeleza kuwa matokeo ya maboresho hayo yanaonekana, akitolea mfano maeneo ya Chalinze na Bagamoyo ambapo kwa mwaka mzima hakuna taarifa ya mwanamke aliyefariki wakati wa kujifungua.
Kwa upande wa Wilaya ya Same, Dkt. Samia amesema tayari serikali imejenga vituo vya afya sita na inaendelea kukamilisha vituo vitatu pamoja na zahanati tano. Aidha, ameeleza mpango wa kujenga vituo vingine vya afya katika kata za Vudee, Mshewa na Makanya.