GE2025 Samia: Hakutakuwa na tishio lolote la kiusalama siku ya Uchaguzi

GE2025 Samia: Hakutakuwa na tishio lolote la kiusalama siku ya Uchaguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mtu anataka kuhalalisha uoga uliopo tayari. Ungekuwa kweli hakuna hofu, basi isingehitajika kutamka hivi.

=================

"Tunaomba kura zenu Wanamsata, la muhimu sana Wanamsata, tarehe 29 mwezi wa 10, Mwenyezimungu tumuombe atuamshe salama, ukitoka kuelekea kituo cha kura, tunasema twende pamoja, mpitie na jirani yako na jirani yako mwambie twende pamoja. Balozi wa nyumba 10 pitia nyumba zako wambieni twende pamoja.

Ninalotaka kuwahakikishia, hakutakuwa na tishio lolote la kiusalama, tumejipanga vizuri mno, hakutakuwa na tishio la kiusalama, asitokee mtu kuwatisha, tokeni mkapige kura, yamewashinda wenyewe kuingia kwenye mashindano wasiharibu upigaji wa kura",- Dkt. Samia.

Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizungumza Msata mkoani Pwani kwenye mkutano wa kampeni Jumapili Septemba 28, 2025.
 
Attachments

  • IMG-20250615-WA0033.jpg
    IMG-20250615-WA0033.jpg
    32.6 KB · Views: 21
, yamewashinda wenyewe kuingia kwenye mashindano wasiharibu upigaji wa kura"
Huyu naona kila mahali anakiona kivuli cha CHADEMA kinacho mtisha sana.
Hajui kuwa waTanzania ndio wameamua kupambana na ujambazi anaolifanyia taifa hili; hata bila kuwepo kwa CHADEMA?
Ninalotaka kuwahakikishia, hakutakuwa na tishio lolote la kiusalama, tumejipanga vizuri mno, hakutakuwa na tishio la kiusalama, asitokee mtu kuwatisha, tokeni mkapige kura
Yeye mwenyewe alijitangaza kuwa "Chura Kiziwi", watu watamuamini vipi kuwa kweli anausikia ukweli unaozungumzwa na waTanzania!

"Mmejipanga vizuri mno"; mtawaweza waTanzania mamilioni kwa mamilioni? Acha wakudanganye hadi hapo dakika ya mwisho, ukibahatika sana utadandia usafiri wa kukupeleka kwa wajomba. Muda wako hapa umekwisha.
 
tunasema twende pamoja, mpitie na jirani yako na jirani yako mwambie twende pamoja. Balozi wa nyumba 10 pitia nyumba zako wambieni twende pamoja
Huyu Jambazi kweli kachanganyikiwa kabisa sasa; hata mbinu za kulazimisha watu kuwapeleka vituoni kazitoa nje nje!

Hao "mabalozi wa nyuma 10" wakithubutu kuhujumu jitihada za wananchi kuukata ujambazi huu, hao hao waonje joto la jiwe siku hiyo 29 Oktoba.

Balozi wa nyumba 10, mtakapo pewa hizo pesa kuleni, lakini msithubutu kuinajisi nchi yetu kwa kuwatumikia majambazi haya.
 
Huyo balozi atamkusanya nani kama ng'ombe aende akapige kura, natulia tu home kwangu bila wasiwasi wanifate na sanduku lao kwangu kama wanataka kura.
 
Sasa unatuletea taarifa hii itusaidie nini,huyo Mama yako sisi hatumtaki,na mwambie aanze kula vizuri tu sasa hivi maana muda si mrefu presha itakuwa juu.
 
Karl Marx
Religion is the opium of the people"

Ndugu watanzania, niwape elimu kidogo,

Taifa Tanzania ni ideology lakini maisha yetu sisi ni uhalisia, tupo kwenye pori kubwa, ambalo kila mnyama anajitadi kujilinda yeye na kizazi chake ili wasogee mbele,

Mungu pia ni ideology lakini maisha yetu sisi ni uhalisia usiopingika na hizi ideology zipo ili kuhakikisha hatuishi kama anavyoishi simba na fisi waliokataa ideology ya Serengeti kutawala vichwa vyao,

Kwenye pori letu leo ubabe ndio njia, sio mgawanyo wa nguvu kama ambavyo ideology ya Tanzania ilitudanganya hapo awali, ni kwanini tuwinde sisi halafu, tulishwe mizoga na tukubali, eti Kwa madai ya ideology ya kipumbavu kuwa sisi ni watu na tupo tofauti na wale wanyama wengine,

Hili pori wanyama wanatoboa kwa kufanyiziana njama, sio kwa kudanganywa na wahuni waliolipwa baada ya kuona sadaka zetu haziwatoshi ili waje watudanganye tuilinde amani ya nchi yetu, I mean our ideology

Ninawahakikishia, hao wazushi hata huyo Mungu ambae huwa wanamzungumzia huwa hawamuelewi zaidi ya kuwaimbia na kuwaigizia baada ya kutonywa kuwa mnyama mtu anapenda sanaa ya muziki na maigizo,

Fisi ni mnyama muoga, ila ndie mnyama anayeogopeka zaidi na wawindaji wa mwituni, huyo mwanamama anawalaghai, ni kwanini katika hili la kutetea maslahi yenu na ninyi msichague kuwa chura mkaachana na kelele za hawa matapeli wa peponi na aliyewatuma,

Gone mad.....
 
29 October, ndo siku aliyozaliwa John Pombe Joseph Magufuli.
What a day.
 
Mtu anataka kuhalalisha uoga uliopo tayari. Ungekuwa kweli hakuna hofu, basi isingehitajika kutamka hivi.

=================

"Tunaomba kura zenu Wanamsata, la muhimu sana Wanamsata, tarehe 29 mwezi wa 10, Mwenyezimungu tumuombe atuamshe salama, ukitoka kuelekea kituo cha kura, tunasema twende pamoja, mpitie na jirani yako na jirani yako mwambie twende pamoja. Balozi wa nyumba 10 pitia nyumba zako wambieni twende pamoja.

Ninalotaka kuwahakikishia, hakutakuwa na tishio lolote la kiusalama, tumejipanga vizuri mno, hakutakuwa na tishio la kiusalama, asitokee mtu kuwatisha, tokeni mkapige kura, yamewashinda wenyewe kuingia kwenye mashindano wasiharibu upigaji wa kura",- Dkt. Samia.

Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizungumza Msata mkoani Pwani kwenye mkutano wa kampeni Jumapili Septemba 28, 2025.
No Reforms No Election
 
Pale unapotegemea wanadamu na kujipa asilimia zote
 
😂😂😂😂 October tunatoka
 
Back
Top Bottom