Akili hizi za kumsikiliza Tundu Lissu na kuwa brainwashed, ni ngumu kuelewa..
Umeusoma ule mkataba vizuri na umeelewa sehemu gani ina tatizo kidogo pa kurekebisa? Sbb ikiwa hujui chochote, bora kukaa kimya, huwezi pata mwekezaji wa kisasa kwenye Bandari kama DP World, ndio kampuni sahihi sana.
Vifungu sana sana viwili au vitatau tu vya kurekebisa,
1: Muda wa Mkataba uwekwe wazi labda miaka 33, kama mkataba utaenda vizuri wataongeza
2: Watu wetu wa TEHAMA nao wawe involved ktk system mpya ya mapato ya Bandari, ili mapato halisi yajulikane na investment cost halisi iwe wazi na tuweze kujua mapato halisi ili serikali ipate haki yake na mwekezaji apate haki yake.
3: Ajira za wazawa ni jambo muhimu sana, kwani Waziri kaweka wazi ajira zitaongezeka, hili ni suala la kuangalia kwa makini, kwani mwekezaji nae atataka watu wake wengi waje wasimamie, hivyo utaratibu mzuri kabisa uwepo wazi juu ya ajira ya pande zote, ni uwekezaji mzuri kabisa, tuache siasa mbovu za kishabiki