GE2025 Samia: Huwezi sikia mtu wa CCM akisema tukiwashe kwa fujo, wakisema tukiwashe ni King'amuzi cha Azam

GE2025 Samia: Huwezi sikia mtu wa CCM akisema tukiwashe kwa fujo, wakisema tukiwashe ni King'amuzi cha Azam

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mgombea urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan, akiendelea na kampeni Kasulu Mjini, Kigoma leo Septemba 13, 2025), amesema chama chake hakina utamaduni wa vurugu.

"Humsikii Mtu kwenye Chma Cha Mapinduzi (CCM), anasema tukiwashe, wakisema tukiwashe ni kile King'amuzi cha Azam, lakini sio tukiwashe kwa fujo,...kukiwasha kwa fujo hapana!"

 
Nilibubujikwa na mqchoz kuona Azam wanapush sana kampeni za mama kwenye match tangazo linaekwa kwenye Big moments...hakika mama ni kipenzi cha Matajiri walala hoi nendeni zimbabwe.
 
Ccm wao ni wanyonyaji wasiopenda kutenda haki, kwa mtaji huo...wakinukishe kwa lipi labda?!.
Siku wakitendewa kinyume kama wanavyotendewa chadema nao watahubiri kuhusu kukinukisha!!.
 
"Niwaombe sana ikifika mwezi Oktoba mwaka huu tuamke mapema kama tulivyojaza uwanja huu, twende tukajaze vituo vya kupiga kura, tukakichague Chama Cha Mapinduzi (CCM), chama kinachojali utu wa mtu. Chama kinachojali ustawi wa taifa letu la Tanzania. Humsikia mtu kwenye Chama Cha Mapinduzi akisema tukiwashe, wakisema tukiwashe ni kile king'amuzi cha Azam, lakini siyo tu kukiwasha kwa fujo, kukiwasha kwa fujo hapana"- Dkt. Samia

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika mkutano wa kampeni ya uchaguzi wilayani Kasulu mkoani Kigoma leo tarehe 13 Septemba, 2025.
 
Back
Top Bottom