Samia Infrastructure Bond, wekeza 500,000/- uvune sh. 15,000/- kila mwezi

Wewe ndio mkurugenzi mkuu?
 
Hivi kwa nini lugha ya kiswahili inataka kuharibiwa sana na matapeli pamoja na machawa hii?

Rais anaitwa Samia, hana mtoto anayeitwa Samia, ana watoto wenye majina tofauti tofauti.

Kiswahili sahihi anaitwa 'Rais Samia'
Kwa wale walamba miguu, mlitakiwa kumuita 'Mama Abdul' na siyo 'mama Samia'.
 
Hah haha haha
 
Hii ni mbinu mojawapo ya CCM
kugharamia uchaguzi mkuu kupitia ukwasi wa CRDB. Lengo la kukarabati miundombinu limekaa kimkakati zaidi ingawa atakayewekeza hatapoteza ila atakuwa amechangia uchaguzi wa 2025
 
Umekosea, kwa hesabu yako inamaana riba kwa mwaka inakuwa 120%. Hii haijawahi kutokea kwenye sayari yetu ya dunia kwenye mifuko ya uwekezaji kutoa kiwango hicho, labda DECI.
Hata hesabu iweje, hii ni biashara kichaa ambayo inaweza kufanywa na mafisadi Papa na wauza madawa ya kulevya ili kutakatisha pesa zao chafu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…