Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 9,524
- 13,682
Rais Samia amewatimua kazi DC na DED wa wilaya ya Mtwara baada ya wananchi wa kata moja kurudisha kadi za CCM kwa sababu ya kuhamisha mradi uliokuwa ujengwe kata hiyo kuhamishiwa kata nyingine kisa uwepo wa wanachama wengi wa vyama vya upinzani.
DC na DED walihamisha mradi wa maendeleo kupeleka kata nyingine ili kuwakomoa wananchi hao kwa sababu wengi wao wanashabikia upinzani. Sasa badala yake DC na DED wametimuliwa kwa kuwakomoa wananchi na Rais amewatimua kwa kuikosesha CCM wanachama!
Magufuli aliwahi kuwatishia ma-DED kuwa endapo watawatangaza wapinzani kushinda chaguzi mbalimbali angewafukuza kazi kisa yeye ndiye aliyewateua! "Niwateue mimi halafu mtangaze mpinzani ameshinda? ........Hiii wangosha!" Magufuli alishangaa.