Samia kukinywea kikombe cha Harris Kamala Uchaguzi Mkuu 2025

Nandagala One

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2020
Posts
1,913
Reaction score
2,286
Heshima kwenu wakuu.

Natanguliza conflict of interest. Mwaka 2025, endapo Kassim Majaliwa hatakuwa mgombea, basi Samia ajiandae kwa yaliyomkuta Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, ambaye alijaribu kugombea urais baada ya Rais Joe Biden kujiuzulu.

Samia alichukua urais kwa kurithi baada ya kifo cha Kambale, na sasa anatarajia kugombea tena mwaka ujao. Lakini, CCM inataka kutoa fomu moja tu!

Hata hivyo, kuna tahadhari kwake Samia kwamba huenda akakutana na hali kama aliyokutana nayo Kamala Harris, japokuwa sababu zitakuwa zinatofautiana kidogo. Hizi ni baadhi ya changamoto atakazokutana nazo:

  1. Tanzania na Afrika kwa ujumla kuna mfumo dume, hivyo atakosa kura nyingi za wanaume, ndani na nje ya CCM.
  2. Asilimia kubwa ya Waislamu wanaoamini mwanamke hawezi kuwa kiongozi hawatampa kura.
  3. Watanzania wengi wanaojitambua hawawezi kumpa kura mtu anayeuza rasilimali za nchi kama bandari na mbuga za wanyama.
  4. Vijana wengi, hasa wahitimu wa vyuo ambao hawana ajira, watapiga kura dhidi yake.
  5. Idadi ya vijana watakaopiga kura kwa mara ya kwanza watachagua upinzani.
  6. Migogoro ndani ya CCM, kama ile iliyosababisha Nape, Makamba Jr, na Mzee Kinana kupigwa chini, ni dalili kuwa hali si shwari ndani ya chama.
  7. Wamarekani, ambao tunaamini ni mfano wa kuigwa katika women empowerment, wamemkataa mwanamke kwa ajili ya jinsia yake licha ya sifa zingine.
  8. Marekani imekataa mara mbili kumpa mwanamke nafasi ya juu; walimkataa Hillary Clinton, na jana wamemkataa Kamala Harris ambaye aligombea kutoka nafasi ya Makamu wa Rais.
Sisi Tanzania ni nani mpaka tusijifunze kutokana na jambo hilo kutoka Marekani?

Salama ya CCM, kwa kiasi fulani, ni kuja na jina tofauti kama la Kassim Majaliwa, ili kupata mwanga wa kushindana na upinzani.

Slogan kuwa "upinzani umekufa" ni uongo na ni kichaka cha kujifariji. Mnakumbuka mlivyotumia nguvu kubwa kuzima maandamano ya chama mnachosema kimekufa.

Kwa heshima na taadhima, Mzee Kikwete, mshauri Mama akapumzike Kizimkazi na alee wajukuu wake.

Samia Suluhu Hassan, nasikia unasomaga JamiiForums. Nakuomba uufanyie kazi ushauri huu wa kutogombea ili uepuke aibu. Zaidi ya hapo, utalazimika kutumia nguvu kubwa, kuua, kujeruhi, kupoteza watu, na kutumbua kwa ajili ya kulinda urais.

Shime! 2025 ni nafasi pekee ya mabadiliko. Binafsi sijali sana chama, ingawa natamani upinzani ushinde. Lakini sio Samia; kumpa urais ni kumpa nafasi ya kuimaliza nchi kwa kuuza rasilimali zake.

Shime Watanzania, tuilinde Tanzania dhidi ya wauza rasilimali za vizazi vijavyo.

Tanzania kwanza, vyama na dini baadaye.
 
Kundi kubwa la uliowataja halijajiandikisha!!wamewaandikisha wanafunzi wengi wasiojua ugumu wa maisha Hadi padre kitima akatema nyongo!

Hizo hizo data ndio watazitumia kumshindisha mama!!
 
Kwamba SSH na Haris, wote walitokea umakamo, wakiutaka Urais kupitia Sanduku la kura.

Si vyema Makamo( msaidizi) kutamani nafasi ya juu na kuacha usaidizi.

Tusubiri.
Naam, Rabbon AKA Bwana, Mwalimu,

Natamani sana atumie busara dakika za Mwisho kutogombea,maana sioni future ya Tanzania chini yake,

Wizi mtupu serikalini, kuliko utawala wowote,

Kakopa sana ndani ya mda mfupi kumshinda Nyerere,Mwinyi,Mkapa, Magufuli, wote kwa pamoja,husu sio wa kumpa nafasi tena!!
 
Kundi kubwa la uliowataja halijajiandikisha!!wamewaandikisha wanafunzi wengi wasiojua ugumu wa maisha Hadi padre kitima akatema nyongo!

Hizo hizo data ndio watazitumia kumshindisha mama!!
Mkuu 2020, ukiona Halima mdee analia,kura amekamata mabegi ya kura feki zilizopigwa na hakuna kilichofanyika.

Shirikisha kidogo ubongo utaelewa ukweli, acha mahaba!!!
 
Kwa chama gani na opponent yupi!?
 
Siyo kwa ccm hii iliyojaa wezi.

Usichokijua huyo Samia siyo kwamba anapendwa hata humo ccm wanamuona ni failure na wanamchukia kishenzi huyu wanaomtaka ni wale waliopo kwenye mlolongo wa upigaji ambao wana ushawishi chamani nje ya hapo asingetoboa hata kura za maoni asingetia pua.
 
Mwanamke awe raisi wa watu wanaojitambua!? Haikubaliki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…