Samia kumteua Dkt. Evaline Wilbard Munisi kuwa Naibu Waziri, kaivunja katiba ya Tanzania

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Ukisoma vizuri Katiba utaelewa ninachosema

Mfumo wa vyama vingi (Ibara ya 10 ya Katiba) unaruhusu vyama kushiriki uchaguzi, lakini chama kinachoshinda ndicho kinaunda serikali. Rais, akiwa kiongozi wa chama kilichoshinda, huchagua mawaziri kutoka miongoni mwa wabunge wa chama hicho. Ibara ya 54(1) na Ibara ya 55(1) za Katiba ndizo zinazoweka msingi wa Rais kuteua mawaziri kutoka chama kilichoshinda uchaguzi pekee.

Kwa Katiba iliyopo Rais hawezi kuteua mawaziri au Naibu mawaziri kutoka vyama vingine, lakini Rasimu ya Warioba ya mwaka 2014 iliweka fursa kwa vyama vingine kushiriki kuunda serikali ikiwa vitapata angalau 30% ya kura za Urais (Ibara ya 97-103 ya Rasimu hiyo). Hata hivyo rasimu hiyo haikupitishwa na Bunge la Katiba na hivyo bado Katiba ya mwaka 1977 inaendelea kutumika.

Soma Pia: Dkt. Evaline Munisi ateuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Ajira na Mahusiano)

Kwahiyo Rais akiteua Waziri au Naibu waziri kutoka chama cha upinzani anavunja Katiba. Lakini anaweza kuteua wabunge hadi 10 kwa mamlaka yake ya uteuzi, ambapo miongoni mwao wanaweza kutoka vyama vya upinzani kama Wabunge wa Kitaifa [Ibara ya 66(1) (e)].

photo_2026-05-02_22-19-55.jpg
 
Umeeandika maandishi mengi ila pumba tupu. Ibara ya 55.-(4) imesema wazi kuwa mawaziri na naibu mawaziri watateuliwa kutoka miongoni mwa wabunge na haijataja kutoka kwa chama chenye wabunge wengi kama ilivyo kwa waziri mkuu. Kuna nyumbu zitaamini haya mashudu uliyoandika kwa sababu zinadai katiba mpya bila kujua kilichomo kwenye katiba ya sasa.
 
Hakuna sehemu katiba haijafuatwa. Wewe ni mpotoshaji. Kwa faida ya nyumbu nimeweka hapa sehemu ya hiyo ibara.

55.-(1) Mawaziri wote ambao ni wajumbe wa Baraza la Mawaziri kwa mujibu wa ibara ya 54 watateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Waziri Mkuu.

(2) Pamoja na Mawaziri waliotajwa katika ibara ndogo ya (1), Rais aweza, baada ya kushauriana na Waziri Mkuu, kuwateua Naibu Mawaziri. Naibu Mawaziri wote hawatakuwa wajumbe wa Baraza la Mawaziri.

(3) Rais aweza kuteua idadi yoyote ya Naibu Mawaziri ambao watawasaidia Mawaziri katika utekelezaji wa kazi na shughuli zao.

(4) Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge.
 
Ukisoma vizuri Katiba utaelewa ninachosema

Mfumo wa vyama vingi (Ibara ya 10 ya Katiba) unaruhusu vyama kushiriki uchaguzi, lakini chama kinachoshinda ndicho kinaunda serikali. Rais, akiwa kiongozi wa chama kilichoshinda, huchagua mawaziri kutoka miongoni mwa wabunge wa chama hicho. Ibara ya 54(1) na Ibara ya 55(1) za Katiba ndizo zinazoweka msingi wa Rais kuteua mawaziri kutoka chama kilichoshinda uchaguzi pekee.

Kwa Katiba iliyopo Rais hawezi kuteua mawaziri au Naibu mawaziri kutoka vyama vingine, lakini Rasimu ya Warioba ya mwaka 2014 iliweka fursa kwa vyama vingine kushiriki kuunda serikali ikiwa vitapata angalau 30% ya kura za Urais (Ibara ya 97-103 ya Rasimu hiyo). Hata hivyo rasimu hiyo haikupitishwa na Bunge la Katiba na hivyo bado Katiba ya mwaka 1977 inaendelea kutumika.

Soma Pia: Dkt. Evaline Munisi ateuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Ajira na Mahusiano)

Kwahiyo Rais akiteua Waziri au Naibu waziri kutoka chama cha upinzani anavunja Katiba. Lakini anaweza kuteua wabunge hadi 10 kwa mamlaka yake ya uteuzi, ambapo miongoni mwao wanaweza kutoka vyama vya upinzani kama Wabunge wa Kitaifa [Ibara ya 66(1) (e)].

View attachment 3583041
Hapana, hizi ibara hazijaweka sharti kwamba mawaziri lazima watokane na wabunge wa chama tawala. Mbunge yeyote anaweza kuteuliwa kuwa waziri. Sharti pekee lililopo ni kwamba Waziri Mkuu lazima awe mbunge wa kuchaguliwa kwenye jimbo la uchaguzi na atokane na wabunge wa chama chenye majority of seats Bungeni, kama kipo. That means upo uwezekano wa Rais na Waziri Mkuu kutoka vyama tofauti, kama chama cha Rais hakikupata majority of seats Bungeni.

Hata hivyo, huyo Munisi sio mpinzani wa kweli. Ni mmoja wa wale political saboteurs waliovalishwa kanzu ya upinzani (i.e., wapinzani kazi maalumu)!
 
Ukisoma vizuri Katiba utaelewa ninachosema

Mfumo wa vyama vingi (Ibara ya 10 ya Katiba) unaruhusu vyama kushiriki uchaguzi, lakini chama kinachoshinda ndicho kinaunda serikali. Rais, akiwa kiongozi wa chama kilichoshinda, huchagua mawaziri kutoka miongoni mwa wabunge wa chama hicho. Ibara ya 54(1) na Ibara ya 55(1) za Katiba ndizo zinazoweka msingi wa Rais kuteua mawaziri kutoka chama kilichoshinda uchaguzi pekee.

Kwa Katiba iliyopo Rais hawezi kuteua mawaziri au Naibu mawaziri kutoka vyama vingine, lakini Rasimu ya Warioba ya mwaka 2014 iliweka fursa kwa vyama vingine kushiriki kuunda serikali ikiwa vitapata angalau 30% ya kura za Urais (Ibara ya 97-103 ya Rasimu hiyo). Hata hivyo rasimu hiyo haikupitishwa na Bunge la Katiba na hivyo bado Katiba ya mwaka 1977 inaendelea kutumika.

Soma Pia: Dkt. Evaline Munisi ateuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Ajira na Mahusiano)

Kwahiyo Rais akiteua Waziri au Naibu waziri kutoka chama cha upinzani anavunja Katiba. Lakini anaweza kuteua wabunge hadi 10 kwa mamlaka yake ya uteuzi, ambapo miongoni mwao wanaweza kutoka vyama vya upinzani kama Wabunge wa Kitaifa [Ibara ya 66(1) (e)].

View attachment 3583041
Katiba ni kijitabu tu
 
Kama mtu aliweza kuua makumi elfu ya Watanganyika, katika kwake ni kitu gani?
 
Katiba haisomwi kifungu kimoja,ukamaliza
 
Ulishaambiwa katiba ni kijikitabu tu.unategemea asome kwa akili hyo.watanganyka tumepatikana
 
Back
Top Bottom