Ukisoma vizuri Katiba utaelewa ninachosema
Mfumo wa vyama vingi (Ibara ya 10 ya Katiba) unaruhusu vyama kushiriki uchaguzi, lakini chama kinachoshinda ndicho kinaunda serikali. Rais, akiwa kiongozi wa chama kilichoshinda, huchagua mawaziri kutoka miongoni mwa wabunge wa chama hicho. Ibara ya 54(1) na Ibara ya 55(1) za Katiba ndizo zinazoweka msingi wa Rais kuteua mawaziri kutoka chama kilichoshinda uchaguzi pekee.
Kwa Katiba iliyopo Rais hawezi kuteua mawaziri au Naibu mawaziri kutoka vyama vingine, lakini Rasimu ya Warioba ya mwaka 2014 iliweka fursa kwa vyama vingine kushiriki kuunda serikali ikiwa vitapata angalau 30% ya kura za Urais (Ibara ya 97-103 ya Rasimu hiyo). Hata hivyo rasimu hiyo haikupitishwa na Bunge la Katiba na hivyo bado Katiba ya mwaka 1977 inaendelea kutumika.
Soma Pia: Dkt. Evaline Munisi ateuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Ajira na Mahusiano)
Kwahiyo Rais akiteua Waziri au Naibu waziri kutoka chama cha upinzani anavunja Katiba. Lakini anaweza kuteua wabunge hadi 10 kwa mamlaka yake ya uteuzi, ambapo miongoni mwao wanaweza kutoka vyama vya upinzani kama Wabunge wa Kitaifa [Ibara ya 66(1) (e)].
View attachment 3583041