Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Bi mkubwa amewambia wanaCCM kama wanavyojaza kwenye kampeni basi wakajaze hadi kwenye masanduku ya kura.
Ila kuna waTanzania nao watatoka kwaajili ya maandamano
=====================
Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema kama ambavyo wananchi wanajitokeza kwa wingi kujaza mikutano yake ya kampeni, vivyo hivyo wajitokeze kupiga kura Oktoba 29, 2025.
Msisitizo huo wa Dkt Samia, unakuja zikiwa zimesalia siku 11, kabla ya Watanzania kupiga kura za kumchagua Rais, wabunge na madiwani.
Dkt Samia ameyasema hayo leo, Jumamosi Oktoba 18, 2025 alipozungumza na wananchi wa Kibaoni, mkoani Katavi katika mkutano wake wa kampeni za urais, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi.
“Naomba sana Oktoba 29, asilale mtu, kila aliyeandikishwa aende kupiga kura,” amesema.