Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!

Kila mtu “mpango wa Mungu” toka enzi za JMK mpaka sasa SSH. Inachosha!! Tunaweza kuwasifia kwa mazuri yao bila kuingiza habari za “ni mpango wa Mungu”.

Mnajitahidi sana kutisha wananchi kwa kutaja jina la Mungu huku mkiwa na hila. Hii ndio ile “Usilitaje jina la Mungu bure” aliyoambiwa Musa na sisi hata leo.

Mmekuwa kama wamisionari waliofundisha Mungu lakini baadae wakatumika kutuliza watu ili ukoloni uingie kwa urahisi!!
 
Ana nia njema ila amesimama kwenye jukwaa bovu(CCM).Hiki chama kimejaa watu wabinafsi na waafidhina kwelikweli ambao wanaamini mawazo yao ndiyo bora kuliko ya watu wengine au vyama vingine.Na ndiyo maana ulimuona Magufuli aliamua kuchukua vijana upinzani ili kujaribu kuleta fikra mpya.Tazama jinsi walivyovuruga mchakato wa katiba mpya kule Dodoma kwa kulazimisha mawazo yao na kupuuza maoni ya Wananchi.Ili nchi ikae sawa ni lazima asambaratishe Msoga gang,sasa ataweza??
 

Huu ni upuuzi tu kama mwingine. Unazungumzia vyama vya upinzani kuwa havibebi agenda za wananchi! Kwa namna nyingine unakiri hapa kuwa CCM ndio haibebi maswala muhimu na unataka upinzani ndio uyapigie kelele. Unakiri CCM haifanyi mambo ambayo ni muhimu!!

Kama CCM ingekuwa inafahamu umuhimu wa mambo uliyoyataja - upinzani usingekuwepo hata!! Sijui kwanini analaumiwa mpinzani asiyekuwa na uwezo wala mamlaka ya kubadili inayoyasema na kumwacha anayeweza kuyabadili!!

Mtakuwa na akili lini???
 
Braza teuzi unaifukuzia kwa speed ya mwanga kwa pambio za tumsifu 😀😀😀
 
Kama CCM ingekuwa inafahamu umuhimu wa mambo uliyoyataja - upinzani usingekuwepo hata!! Sijui kwanini analaumiwa mpinzani asiyekuwa na uwezo wala mamlaka ya kubadili inayoyasema na kumwacha anayeweza kuyabadili!!

Mtakuwa na akili lini???
Upinzani haujawahi ongelea hayo niliyoongelea popote

Wao wamebeba tu agenda za viongozi tu mfano wanataka tume huru itayokuwa na viongozi wa vyama vyote wanatafuta uongozi !! Ndani ya tume!!

Yale wanayohitaji wananchi hakuna chama hata kimoja cha upinzani kinaongelea Kero halisia za wananchi na kuzivalia njuga.Utakuta tu wanaibuka kipindi tu cha uchaguzi na porojo zao hewa za ohh tukishika tutafanya hivi.Na hizo porojo zao nyingi hata hazigusi matatizo halisia ya wananchi
 
Akafie huko hana lolote. Kaja kutuharibia tanzania yetu ya kijamaa kuleta walamba asali kushika dola.
 
Yaaaaaawn!! Hata kesho rais akiwa Rungwe au Mosses Machalii utasema hayo hayo ili mradi upate matangazo ya serikali
 
Kweli miaka imeenda na nchi yangu imebadilika. Nyerere alikuwa Rais wa Tanzania kwa miaka 21 lakini hata siku moja hatukumuita Mheshimiwa ingawa alistahili na alipewa heshima zote. Tulimuita Ndugu kama vile tulivyowaita hata wale waliokuwa wanafagia ofisi zetu. Hatukumuita Dr ingawa alikuwa na Ph.D za heshima kibao. Tulimuita Mwalimu maana ndivyo alivyotaka aitwe na aliona ndio sifa anayostahili. Na zaidi ya yote hatukudiriki kumuita kuwa yeye ni Mpango wa Mungu kwa sababu tulijua yeye ni binadamu wa kawaida ambae tuliabudu pamoja kanisani na siku ya mwisho atahukumiwa kama sisi sote kwa namna alivyoishi maisha yake.
Miaka hii mbali ya kumuita mtu tuliyemchagua kuwa ni mpango wa Mungu kuna wakati tunaenda mbali zaidi na kumuita Mungu.
Nyerere huko aliko atakuwa anasononeka vibaya sana.

Amandla....
 
Awamu ya 4 Chini ya JK demokrasia ilishamiri hadi baadhi ya viongozi wa siasa wakadiriki kudhihaki Serikali yake.
Sheria zilizo kuwepo ni hizihizi na wanasiasa walijimwaga sana.......hivyo tatizo sio sheria bali ni utashi wa kiongozi aliyepo.

awamu ya 6 chini ya Mama kama kiongozi Mkuu kaonyesha utashi wa hali ya juu wa kuweka mazingira sawa na rafiki kwa wanasiasa.......

Jambo la msingi la kuzingatia ni kwamba Demkrasia ya Marekani au nchi nyingine haiwezi "kufit" kwenye mazingira ya nchi yetu.

Ndio maana mchakato wa katiba mpya ulikwama, bado wana siasa wetu wa vyama pinzani ni wachanga mno.....

tusijaribu kuipaka awamu 6 mafuta kwa mgongo wa chupa ili kufanikisha kupenyeza mambo ya wanasiasa wachache wenye uchu wa uongozi, kama kuna jambo lenye masilahi kwa siasa zetu basi vyama vyote vya siasa vishirikishwe na vitoe maoni yao kisha maamuzi yafanyike.
 
Siyo Paul Makonda tena? Maana uliandika kuwa baada ya Magufuli basi Makonda anaweza kuwa Rais bora
 
Ujinga wetu ndio unawafanya akina Pascal kutuaminisha Mungu anamakazi yake Tanzania tu ili utupe marais wabovu wanaotupa chokoleti badala ya ndoano. Pascal anajua sisi na Indonesha tulikuwa sawa kutawaliwa na umasikini ila wenzetu walichagua viongozi wazuri waliowapa ndoano na kuwanyima chokoleti, hivi sasa wako mbali sana kimaendeleo huku sisi tuko kwenye kuiba kura ili tutawale zaidi ya miaka 80 ijayo kama alivyojitapa Polepole.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…