Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!


 Mungu hana ushirika na wanasiasa ndugu.
Labda awe mungu wa dunia hii...
 
Baba mkubwa naona umeshamaliza kazi. Sasahivi umekaa unasubili teuzi tu. 😆😆Tz raha sana, kutoboa hakuitaji nguvu nyingi
 
Pascal Mayalla umeandika vitu viingi lakini hoja yako haijulikani imesimama upande gani!🤔🤔
Mkuu Mwizukulu mgikuru, sio kila hoja ina upande. Hapa nimezungumza mambo 4 na hayana upande!.
1. Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania.
2. Kuna jambo amelisema, akilitekeleza Atabarikiwa na Tanzania Itabarikiwa
3. Kumshukuru Mungu kwa Samia
4. Kumuombea na kuliombea taifa.

Hapo kuna issue gani ya upande?.
Maandishi ni kama binadamu, wengine wakubwa, wengine wadogo, wengine wanene, wengine wembamba, wengine warefu wengine wafupi, hivyo maandishi ni kama binadamu mengine makubwa, mengine madogo, mengine marefu, mengine mafupi, mengine magumu, mengine marahisi, ukiona, umesoma kitu halafu huelewi, ujue maandiko hayo sio saizi yako, yatakuwa yamekuzidi Kimo. Pole!.
P
 
Mataifa ya Africa ni KAZI kuendelea Kwa sababu ya uwepo WA viumbe wengi jamii ya Pascal.
 

Naona hukusoma mada yangu na kuielewa. Ni mpaka wananchi wa aina yako watakapopungua kwa idadi ndio nchi hii itasonga mbele!!

Nakukumbusha - hayo unayoyasema yangekuwa ni ya muhimu kwa CCM, wangeyafanya na kungekuwa hakuna haja ya upinzani! Jua unayemlaumu hapa kwa kutobeba mambo ya wananchi ni CCM. Unayemlaumu anatafuta nafasi ya kuwa madarakani ili ayafanye au ayapuuze kama CCM. Anatafuta namna ya kuingia na kuwa na mamlaka ya kutenda!! Kwa sasa hata akiyapigia kelele, anamwambia CCM - ndiye mwenye mamlaka!! Ingekusaidia sana kutoa mfano wa jambo gani wapinzani waliwahi kupigia kelele na CCM ikalifanya!!!!

Mfumo wa uongozi wa kidemokrasia unampa mamlaka anayeongoza na kuwa madarakani aliyechaguliwa kwa kura kuzidi washindani wake!! Sio vinginevo!! Na ndio maana vyama hivi vinashughulikia “tunaingiaje madarakani”!!!

Ni aibu kuwa hufahamu jambo dogo kama hili - na miaka yote hiyo ya umri, na kitambi na ndevu zote hizo!!
 
we jamaa bana hata huelewekagi unataka nin! halafu kama unatumika kwa ajili ya kuangalia upepo huwa unafeli sana mahali pa kuanzia
Mkuu Mtemi mpambalioto, rukhsa kuhisi lolote, hiyo ni haki yako.

Mimi ni Mwandishi tuu wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, situmiki na yeyoye, najituma mwenyewe.

P
 
Well said Paskali. Huyu mama ameanza vizuri sana, aongeze mwendo, tutafika tu.
 
Hatusemi asante Mungu kutuondolea JPM na kutuletea Samia
You can't have it both ways
Kwani kuna ubaya gani kumshukuru Mungu kwa kumchukua mja wake JPM?
JPM alikuwa binaadamu na sio malaika, yale mambo ya kibinaadamu yasiyotupendeza enzi za JPM, tuyaache, tusiendee kuyasema sema ni kama kumsimanga marehemu, tumuache JPM apumzike kwa amani
JPM alimsema Nyerere kwa kusaidia ukombozi. Alimsema Nyerere kwa uhusiano na Israel na mengi tu

JF Mwalimu amejadiliwa miaka 23 tangu afariki , hatukusikia haya ya 'marehemu hasemwi'
Tunamkosoa Nyerere kwa sera zake , Ubinadamu na Utu wake unamlinda bila kuhitaji utetezi akiwa kaburini

JPM ni Marehemu tu kama Mkapa na Nyerere, tutayaeleza yake mazuri na yale mabaya bila kupepesa

Hizi habari za marehemu hasemwi ni kwa kutambua kuwa katika hazina zake kuna tatizo , tunataka afichiwe

No! watu waeleze kila kitu ili tujifunze tusijefanya makosa mengine yatakayotugharimu miongo mingi ijayo

Nashukuru ujio wa JPM. Urais wake umetuonyesha kile wenzetu wa mataifa hasa Afrika walichokilalamikia
Miaka ya 70,80 nchi za Afrika zilitumbukia katika machafuko na Mapinduzi kila uchao, Tanzania hatukujua ni kwanini

JPM alituonyesha kwa uwazi hisani za watangulizi wake na kutufunulia matundu ya katiba ya nchi
Alituonyesha jinsi mtu mmoja na kundi la vijana akina Sabaya na Bashite wanavyoweza kutesa nchi
JPM alitufunulia mengi sana tuliyokuwa hatuyajui hasa ubovu wa mifumo ya nchi ikiangukia mikono mibaya
JPM ametuachia nyufa za mbegu za udini na ukabili vitu tulivvyodhani Tanzania haikuumbwa navyo
JPM akatuonyesha kiongozi anavyoweza ku 'hypnotize ' Taifa

Bila yeye tungeyajuaje hayo? Bila yeye tungejifunzaje ?
 
we jamaa bana hata huelewekagi unataka nin! halafu kama unatumika kwa ajili ya kuangalia upepo huwa unafeli sana mahali pa kuanzia

unawakilisha watu wanaojihita wanademokrasia lakini maneno na matendo yao Ni kinyume. JF —- we dare to speak. Je umezingatia uhuru wa mwenzako? Kwanini unataka kumpangia. Je. Unataka amsifie mbowe Labda ndo utakuwa msosi na sio uharo.
 
Umemalizia vizuri sana 1- Haki huinua Taifa ! 2- Rais Samia anazidi kuthibitisha yeye ni chaguo la Mungu kwa Tanzania ! 3 - NA AKITEKELEZA HAYA RAIS SAMIA ATABARIKIWA NA TANZANIA ITABARIKIWA !! kweli kabisa hata Mimi naunga mkono 100%, sasa tusubiri tuone kwanza !!!
 
Hivi ni lini nchi yetu itapata wazalendo wa kweli wanaoweza kupaaza sauti zao?? Licha ya kona nyiingi ila hoja ni kumsifia Chifu Hangaya.
 
Na hivyo ndivyo ilivyo, lakini tusubiri kwanza tuone ni dhamira ya kweli ambayo vitendo vyake vitadhihirisha hiyo dhamira ?! Au itakuwa ndiyo yale yale maneno ya sii-Hasa ?? Time will tell !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…