Samia ni Rais wa Watanzania Wote Tunamuhukumu kwa matendo na siyo Dini yake

Samia ni Rais wa Watanzania Wote Tunamuhukumu kwa matendo na siyo Dini yake

The Burning Spear

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
4,118
Reaction score
9,864
Kwa ufupi kabisa sakata la DPW ni ukiukwaji wa wazi wa sheria na katiba ya nchi yetu.

Ndiyo maana hata wanaopinga wanataja vifungu vya sheria ambavyo vimekiukwa.

Sasa wale wenzetu wa upande wa pili sisikii wakitaja vifungu chochote cha sheria kuutetea mkataba kwamba ni halali bali na kuongea vitu visivyoeleweka...

Tulipofika siyo pazuri hata kidogo. Na hali itazidi kuwa mbaya zaidi kadri tunavyosonga mbele. Ni jambao lililowazi kwamba serikali ilijichanganya kwenye hili

Mpaka sasa samia kaligawa taifa vipande vipande kinyume na kiapo chake. Hii onatufanya tuamini nje ya mkataba huu kuna mambo mengine meusi ambayo hatuyajui pengine wakubwa yamewakaba koo.


Kamati ya bunge
TLS. Mahakama na sasa Maaskofu wote wanasema mkataba una matatizo afu mjinga mmoja anasema ooh kisa raisi ni muislam ndo maana wapingaji wengi how. Wakati mambo yako wazi kabisa wamekosea.

Raisi wa Tanzania haongozi waislam pekee. wakae wakijua hilo ni raisi wa wote(wazinzi/Makahaba/walevi/wakristo/ wapagani/waislamu na kila aina ya binadanu na anajukumu la kulinda Rasiliminali zetu na siyo kwa ajili ya waislamu. Na pale anapofanya mambo yasiyoeleweka lazima akanywe kwa ukali na nguvu...

Sakata la DPW halina tofauti sana na lilie swala la OIC mara mahakama ya kadhi. Waislamu huwa wanabweteka sana mara Raisi muislamu anaposhika madaraka. Magufuli aliwapenda sana waislamu. Aliwatendea mambo mengi makubwa.

Kinachowasumbua waislamu wengi ni ubinafisi hakuna kingine
 
Na ndiyo maana wanasiasa wenzake wa upinzani wanamkaanga bila kujali mambo yao ya kibinafsi aliyowafanyia. Hata hao wapinzani wasilaumiwe kwamba hawana shukrani kwa wema waliofanyiwa kwa kuwa hayo mambo ilikuwa ni ya kibinafsi na hao wapinzani hawezi kuleta mambo yao ya kibinafsi wakijua wanaongoza wananchi wengi. Nje na huu mnyukano ni marafiki na ndugu wa kushibana na kutendeana mema. Kwenye siasa ni ligi tu hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu ni mnyukano tu ukionesha udhaifu wa kiongozi na katika kujenga hoja jambo lako la kisiasa likubalike
 
Back
Top Bottom