Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeanzisha program ya ufadhili iitwayo SAMIA SCHOLARSHIP kwa masomo ya shahada ya kwanza kwa wanafunzi waliopata ufaulu wa juu katika mitihani ya kidato cha 6 mwaka 2022 chini ya NECTA kwa waliosoma masomo ya;
PCB,
PCM,
PGM,
CBG,
CBA,
PMC,
CBN
SAMIA SCHOLARSHIP itagharamia kwa Asilimia Mia Moja (100%) katika fani za Teknolojia, Uhandisi, Hisabati na Tiba;
Ada ya mafunzo
Posho ya Chakula na Malazi
Posho ya Vitabu na Viandikwa
Mahitaji Maalumu ya Vitivo
Mafunzo kwa Vitendo
Utafiti
Vifaa Saidizi kwa Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalumu
Wadau Hivi hakuna mtu anayefahamu vyuo/mahala wanapotoa scholarships za masters iwe ndani au nje ya nchi kwa upande wa accounting, economics or finance related degrees?