Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
SAMIA SCHOLARSHIP
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeanzisha program ya ufadhili iitwayo SAMIA SCHOLARSHIP kwa masomo ya shahada ya kwanza kwa wanafunzi waliopata ufaulu wa juu katika mitihani ya kidato cha 6 mwaka 2022 chini ya NECTA kwa waliosoma masomo ya;
PCB,
PCM,
PGM,
CBG,
CBA,
PMC,
CBN
SAMIA SCHOLARSHIP itagharamia kwa Asilimia Mia Moja (100%) katika fani za Teknolojia, Uhandisi, Hisabati na Tiba;
- Ada ya mafunzo
- Posho ya Chakula na Malazi
- Posho ya Vitabu na Viandikwa
- Mahitaji Maalumu ya Vitivo
- Mafunzo kwa Vitendo
- Utafiti
- Vifaa Saidizi kwa Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalumu
- Bima ya Afya