Boya wewe, Kigwa hizo propaganda alizokutuma Kakurwa kuja kuzifanya JamiiForums zimefeli, mtu mwenyewe umejiunga week iliopita JF 09/04/2021.
Jiandae, takukuru wakimalizana na Kakoko jumatatu wakimfikisha mahakamani ujue wanakuja kwako, zamu yako imefika kushughulikiwa.
1) Rais Samia hajamaliza hata "MWEZI NA NUSU" ushaanza kusema ameshindwa kutupa katiba mpya.
2) Rais Magufuli alifukuza mafisadi ili afisadi nchi yeye peke yake. Nchi haijawahi kuwa na Rais muongo na mbaguzi wa kikabila aliopitiliza kama Magufuli.
3) Rais Magufuli ndio ameongoza kwa kuwa Rais wa muda mfupi kuwahi kutokea Tanzania, ila ndio Rais alioongoza kwa kuipa hasara na madeni nchi.
MATAGA hata mfanye nini, tarehe 30/04/2021 Rais Samia ndio anakuwa Mwenyekiti wa CCM, hata mfanye propaganda gani za kumnyima 100% ya kura, yeye ndio atakua Mwenyekiti. Mtake msitake.
Hii itakua bingo kwa wapinzani, maana Rais Samia ni mtu pekee ambae ana "AKILI TIMAMU NA MUELEWA" katika chama kizima cha CCM.
● Raia wamelia na kupanda kwa bei za internet siku moja tu, kalishughulikia.
● Raia walikua hawana furaha na nchi yao, siku moja tu baada ya yeye kuapishwa furaha imerudi.
● Raia walikua wanachukiana kwa itikadi za vyama vya siasa, siku moja tu baada ya kuapishwa mpaka wanachama wa upinzani wanamuunga mkono.
● Raia wamepiga kelele za ufisadi hazina, siku moja tu baada ya kukabidhiwa report na CAG kalishughulikia na linafanyiwa kazi.
● Raia na Vyombo vya habari walikua wanalalamika kukandamizwa na kuonewa kwasababu ya kuikosoa serikali, ameamrisha vyombo vya habari vilivyofungiwa vifunguliwe. Sasa watu wanaikosoa serikali kistaarabu.
MPAKA JAMIIFORUMS tokea Mama Samia kuapishwa tu tumerudishiwa uhuru wa kuikosoa kisawasawa serikali, hasa kumkosoa Jiwe na serikali yake. Hakuna ban wala kufutiwa uzi siku hizi. Huu ndio uhuru tunaotaka.