Uchaguzi 2020 Samia Suluhu: Hata mkipigia kura kule kwingine CCM ndio inaenda kuunda Serikali, tutashinda vikubwa sana Tanzania

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
Your browser is not able to display this video.

Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, (CCM), Mh. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 15/10/2020 amewambia wakazi wa Chunya mkoani Mbeya kuwa wasipige kura kwa Chama Kingine kwa sababu hata wakipiga kwingine Chama Cha Mapinduzi kinaenda kuunda serikali.

Amesisitiza kuwa watashinda vikubwa sana Tanzania, na amefananisha kupigia kura kwa chama kingine kama kitendo cha kumwaga sukari Ziwa Viktoria na kutegemea maji yatakuwa matamu, ambacho ni sawa na kupoteza sukari yako.

Mh. Samia amesisitiza kuwa maendeleo watakayoyaleta sio kwa wana CCM peke yake na wale ambao hawatokipigia Chama Cha Mapinduzi basi kura yao itawasuta pale watakapokuwa wanaletewa maendeleo.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Nape Nnauye: Kauli ya "Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza" ilikuwa ni ya utani

- Dkt. Bashiru: Aliye na dola ndiye ananufaika nayo kubaki madarakani, hata CHADEMA ikiingia madarakani ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wao
 
Duh...
Kuna nini lakini

She shouldn't have said that line.

Kauli hii kama wanajua wataunda serikali kwanini wafanye kampeni.

Alafu hayo maendeleo yanayo yanayozungumzwa kwa zaid ya miaka 60 na CCM hii hii ni yapi.
 
Sasa kama kura zikiwa nyingi kwa chama kingine wao watashinda vipi?

Hii ndo ishara ya kwamba Uchaguzi wetu hauamuliwagi kwa wingi wa kura za halali za kwenye maboksi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…