Wakati wa sherehe ya kukabidhiwa katiba inayopendekezwa nilijisikia aibu ambayo nina miaka mingi kujisikia aibu namna ile. Ukweli ni kwamba awamu hii ya utawala ndo tumeona nchi yetu inaongozwa kwa masihara sijawahi kuona.
Kikwete alimuuliza Samia Suruhu " hivi 2/3 ya bara ilikuwa wajumbe wangapi?" kamera ikamuonyesha Suluhu ameangalia juu akichezesaha vidole kama anahesabu hivi! Mara kamera ikatuonyesha waliokuwa makatibu wa Bmk kama wanajadiliana kitu wasichokuwa na hakika nacho. Mara Kikwete akasema "nadhani kama 350 hivi"!
Yaani suala kubwa kama hili Kikwete, Suluhu, makatibu wa bunge na Sitta mwenyewe hawajiu 2/3 ya bara ilikuwa ni ngapi? Mnaandaa sherehe kubwa kama ile wakati hamna rekodi kamili ya matokeo? hapana, huu ni mzaha na aibu kubwa sana! Katika 'mawimbi na tsunami' aliyosema rais unaweza kufanya mzaha wa namna hii!
Tanzania!!!