Samia suluhu, Makatibu wabunge wamesahau 2/3

mpk

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Posts
3,115
Reaction score
3,864
Wakati wa sherehe ya kukabidhiwa katiba inayopendekezwa nilijisikia aibu ambayo nina miaka mingi kujisikia aibu namna ile. Ukweli ni kwamba awamu hii ya utawala ndo tumeona nchi yetu inaongozwa kwa masihara sijawahi kuona.

Kikwete alimuuliza Samia Suruhu " hivi 2/3 ya bara ilikuwa wajumbe wangapi?" kamera ikamuonyesha Suluhu ameangalia juu akichezesaha vidole kama anahesabu hivi! Mara kamera ikatuonyesha waliokuwa makatibu wa Bmk kama wanajadiliana kitu wasichokuwa na hakika nacho. Mara Kikwete akasema "nadhani kama 350 hivi"!

Yaani suala kubwa kama hili Kikwete, Suluhu, makatibu wa bunge na Sitta mwenyewe hawajiu 2/3 ya bara ilikuwa ni ngapi? Mnaandaa sherehe kubwa kama ile wakati hamna rekodi kamili ya matokeo? hapana, huu ni mzaha na aibu kubwa sana! Katika 'mawimbi na tsunami' aliyosema rais unaweza kufanya mzaha wa namna hii!

Tanzania!!!
 
Mkuu hawa jamaa ni washenz sana hili picha wanalocheza bila mdosi litawadodea wewe waache mungu anawaona.
 
Huwezi kuamini kama watu wazima wanaweza kufanya mazingaombwe haya!
 
Yaan tena ya wazi wazi huku nahodha wao juha akijinasibu kabisa eti akidi isipotimia itatimilizwa tu,

Halafu hata wale waliopga kura ya siri ni wanafiki na walikua wanajijengea mazingira ya kupewa rushwa mwisho wa mchezo kura ziwe ndiyo!
 
AG wa Zanzibar amesema kuna siku ukewli utajulikana! Haiwezekani kila ibara kura za hapana kati ya zile za siri ziwe mbili. Kuna utata hapo.
 
Ndugu tujue kuwa swala hili limekuwa gumu kwani kumekuwa na idadi ya wajumbe tofauti tofauti Rais alikuwa na wajumbe wake lakini pia sita naongozi wake walikuwa na wajumbe wao hewa
Hivyo isingekuwa rahisi kwake rais kuitambua hiyo theluthi mbili bila kuuliza kwani cha ajabu hii 2/3 ya sita na wenzake hatakuiandika kwenye hutuba ilikuwa haitoshelezi
 
Kwa maana hiyo bunge limetupendekezea katiba bila ya kuwa na matokeo ya bara? kama ni hivyo, uharali wake uko wapi? Unaweza kulipwa kiasi hicho cha mamilioni ukaja nusu nusu kwa suala muhimu kama hili?
 
hiyo ni laana asilimia kubwa ya viongoz wana laana ya watanzania kwa kutuibia na kutunyima haki zetu za msing
 
Mwaka huu mapaka mtaugua ugonjwa wa Mshituko wa Moyo (Heart Attack)!

Kwa sasa mnatafuta sindano kwenye mchanga wa baharini!
 
Asante kwakua tutaugua lakini hatutakufa na tukipata nafuu sisi wazee wote kama nyinyi mtakua mshaiacha tanzania yetu nasema mtaugua na kamwe hamtapona!
 
Hivi kwa nini kuna option ya ku-like post na hakuna ya ku-dislike? Kuna posts nyingine nakutana nazo ambazo ninatamani sana kuzi-dislike lakini nashindwa.
 
  • Thanks
Reactions: ffn
Nilishanga Sana na ukweli ni kwamba Mungu ndiye muweza wa kila jambo na anawaumbua wanafiki wazi wazi
 
Wamezoe hesabu za kuchakachua za halali hawawezi wakazikumbuka.
 
Wakati wa sherehe ya kukabidhiwa katiba inayopendekezwa nilijisikia aibu ambayo nina miaka mingi kujisikia aibu namna ile. Ukweli ni kwamba awamu hii ya utawala ndo tumeona nchi yetu inaongozwa kwa masihara sijawahi kuona.

Kikwete alimuuliza Samia Suruhu " hivi 2/3 ya bara ilikuwa wajumbe wangapi?" kamera ikamuonyesha Suluhu ameangalia juu akichezesaha vidole kama anahesabu hivi! Mara kamera ikatuonyesha waliokuwa makatibu wa Bmk kama wanajadiliana kitu wasichokuwa na hakika nacho. Mara Kikwete akasema "nadhani kama 350 hivi"!

Yaani suala kubwa kama hili Kikwete, Suluhu, makatibu wa bunge na Sitta mwenyewe hawajiu 2/3 ya bara ilikuwa ni ngapi? Mnaandaa sherehe kubwa kama ile wakati hamna rekodi kamili ya matokeo? hapana, huu ni mzaha na aibu kubwa sana! Katika 'mawimbi na tsunami' aliyosema rais unaweza kufanya mzaha wa namna hii!

Tanzania!!!

Wajumbe wa bara walikuwa 411 hivyo 411 x 2/3 unapata ni 274. Kwa upande za Zanzibar walikuwa 219 hivyo 2/3 inakuwa ni 146. (kwa mujibu wa hotuba za siku ya kutangaza matokeo?
 
Back
Top Bottom