Samia tumaini jipya Tanzania: The Economist baada ya kumsakama sana Magufuli, sasa angalau lina matumaini na Samia, laanza naye vizuri

Ukweli unaotaka niukubali ni upi?
Nimeona watu wangu wa karibu wakiugua corona na nimethibitisha kuwa mwafrika akichukua tahadhari hana sababu ya kuiogopa corona.

Kwahivyo lazima Africa iwe na njia zake za kukabili maambukizi ya corona tofauti na za wazungu.

Ndio msingi wa hoja yangu ya TUSIPANGIWE.
 
Tunawaza tofauti. Mimi nawaza maslahi ya nchi kwa ujumla wake.
Huwezi kufikiri uchumi kwa ujumla wake bila kufikiri sera za uchumi zinazotengenezwa na mtu
Kwa mfano, TRA, BoT , TIC na vyombo vyote vya uchumi husikiliza sera za aliyeko madarakani
Kwa nchi zilizoendelea , yes, kwa nchi masikini zisizoheshimu taasisi kama yetu huwezikutenga uchumi na mtu
Yaani, ni kitu gani au sera gani ineleta impact ya kiuchumi kwa watanzania kwa ujumla wao, wewe unawaza mtu.
Nimejibu hapio juu. Kwa kuongezea tu, tulikuwa na sera ya uchumi wa soko huria wakati wa Mwinyi, Mkapa na JK.
JPM akaja na sera za 'monopoly' kama tulivyoshuhudia sekta ya anga ambako ushindani uliondolewa.
Unawezaje kutenga uchumi na mtu?
Sheria ya mihimili kutoshtakiwa haina shida.
Siyo mihimili bali wakuu wa mihimili ambao ni wanadamu. Mihimili ni taasisi
Tatizo lako unawaza mtu binafsi badala ya mhimili.
Yes kama mtu huyo ana impact kwa mhimili. Miaka 5 tumeshuhudia mhimili '' uliojichimbia chini zaidi' ulivyo fanya ''redundancy'' kwa mihimili mingine. Hayo hayakutokea katika mfumo wa taasisi na taasisi bali impact ya mtu katika taasisi.
Haina shida mhimili wa uraisi kutoshtakiwa. Urais ni alama ya utaifa, kushtaki urais ni kujishtaki kama taifa. Rais, kama mtu, akiwa mbovu kuna solutions zake. Ya kwanza ni kuwa voted out of the office. Ya pili ni kumaliza muhula na kusepa zake.
Urais ni institution lakini kuna Rais ambaye ni kiongozi wa taasisi.
Rais anaweza kushtakiwa kwasababu yeye pekee si alama bali anabeba alama.

Kuondoka kwa Rais hakuifanyi taasisi kuondoka. Kwa mantiki hiyo Rais anashtakiwa tofauti na mawazo ya kijinga kwamba ni alama. Kote duniani Rais akienda nje ya misingi ya kazi anashtakiwa.

Kilichotokea wakati wa nyuma ni baada ya kubaini kuna mpinzani alishinda kesi hivyo serikali ikapeleka mswada haraka wa kumkinga Rais aliyepo na si Marais waliotangulia. Hii haikuwa sahihi.

Kutengeneza sheria za kujilinda ni dalili ya kuhisi uovu. Hivi unaogopaje mahakama kama wewe ni clean?


 
Mimi nimeona ni-'copy' tu haya:

Mosi, kukupa pole wewe binafsi, kama kimya kile kilikuwa kinatokana na kazi maalum, badala ya uteuzi wa waziwazi, au hata kama kulikuwa bado kuna subira za matumaini ya uteuzi chini ya Magufuli, bahati mbaya sana hilo halikuwa.

Pili - ndiyo, watu wasianze kujipendekeza kwa Samia na kumpa sifa hata kwenye mambo ambayo bado hajayafanya. Hii ni kutaka kujionyesha na kujipitishapitisha tu uonekane machoni au usikike masikioni mwake au kwa wapambe wake.

Tabia hii siyo nzuri hata kidogo, na ilikuwa moja ya tabia zilizomharibia Magufuli. Kupenda sifa kuliko uhalisia wake.

Msitafute kumsukumizia Samia naye aingie huko. Mwache achape kazi za waTanzania ajuavyo inafaa.

Kama ni lawama zitakuwa ni zake, kwa vitendo vyake, msianze kuchochea kwa ushangiliaji wa kkinafiki.
 
Yes kama mtu huyo ana impact kwa mhimili. Miaka 5 tumeshuhudia mhimili '' uliojichimbia chini zaidi' ulivyo fanya ''redundancy'' kwa mihimili mingine
Na kiuhakika zaidi, haukuwa "mhimili uliojichimbia chini zaidi", ni mtu binafsi mwenye mabavu zaidi aliyekuwa anauendesha mhimili huo peke yake, mbali na kuiendesha mihimili mingine alivyopenda.

Utawala wa namna ile haujapata kutokea na sidhani kuwa utatokea tena katika miaka ya hivi karibuni.
 
Waliokua wanatuma makala the economist wanafahamika.

Rais asikubali kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.

Sifa hizo zina malengo ya kujaribu kulegeza misimamo iliyokata mirija ya kinyonyaji.

Namshauri Rais alinde masilahi ya Nchi asikubali kuyumbishwa na mabeberu.
 
Mlimuweka jela bwana Erick kabendera bila hata sababu za msingi kisa the economist.
Wasukuma watu wa hivyo sana.
Bora mungu ameingilia kati shwain
 
Mfumo imara siyo mtu mmoja, ajiimarishe awe mbinafsi na imara!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Mabeberu watukome na wamkome vilivyo mama yetu! Hili gazeti La The Economist likome!! Hamu na tarajio kubwa la mabeberu ni kutuingiza kwenye utumwa wa Corona!! Tanzania ni nchi pekee duniani ambayo imegoma kuwekwa kwenye utumwa wa Corona!! Wazungu na ujanja wao wote wako kwenye kongwa la utumwa wa Corona!! Majirani zetu pia wako kwenye utumwa wa Corona! Kuingia kwenye utumwa wa Corona ni hiari! Lakini ukiingia humo si hiari tena kutoka!! Chonde chonde mama yetu, tafadhali usikubali kutuingiza kwenye utumwa huu wa corona!! Corona is over-rated!! Kila anayekufa wanalazimisha kuwa amekufa na corona ilí kuuhadaa ulimwengu kuwa corona ni ugonjwa hatari Sana!! Siyo kweli!! Hata walio na corona wakifa si kwamba wameuliwa na corona!! Mabeberu wanalazimisha kuwa ukiwa na corona halafu ukafa ni corona imekuua wakati si lazima iwe hivyo!! Tanzania tuko vizuri na wanajua hivyo! Hata Uingereza wametangaza kuwa kuanzia June wataachana na lockdown milele japo maambukizi bado wanayo mengi tu!! Wameamua Jambo hilo wakati Magufuli aliliamua toka awali, lakini bado wanasema Magufuli alifanya kosa! Lakini hawasemi Uingereza inafanya kosa!
Mpango wa chanjo wa covax hauna maana yoyote! Lengo ni kutuweka katika utumwa wa Corona tu!! Chini ya mpango wa covax ni asilimia 20 tu ya watu watakaochanjwa!! Hii ni asilimia ndogo Sana na haisaidii kufikia kuikinga jamii yaani kufikia herd immunity. Herd immunity inaanzia walau kuchanja asilimia 60.
Mabeberu wameshaishiwa rasilimsli za asili! Wameona corona ni biashara ya kudumu!! Wanakukopesha pesa ya kupima corona halafu unailipa kwa riba!! Watukome!!
Mask ina msaada kidogo Sana wa kumkinga mtu kutokuambukizwa!! Ingekuwa na msaada mkubwa basi maambukizi mapya yangeshakoma kwenye nchi ambazo watu wake wanashinda na barakoa!! Lakini huko huko ndo kila siku wanatangaza maambukizi mapya kwa maelfu!! Watukome!! Mama yetu mpendwa tafadhali usituingize kwenye utumwa huu wa corona!! Ila nikupongeze mama, mabeberu tayari umeshawakatisha tamaa!! Walitamani Sana wakuone unashinda na barakoa!! Nikupongeze mama mpaka hapo!! Wasikutishe!! Wasikufanye mtumwa!! Wewe ni Rais huru!!
 
1. Hayati JPM alihakikisha anasimama Imara ktk kulinda Rasilimali zetu haswa Madini alifanya hivyo kwa kubadilisha sheria mbali mbali na serikali ikaanza kunufaika kwa kiasi kikubwa, hatua hii haikuwa rahisi hata kidogo, mabeneru ambao ndio wanyonyaji wakuu kupitia makampuni yao hawakufurahiswa na hatu hizo.
choko choko na chuki ziliibuka.

2. Urafiki wa Mabeberu/wanyonyaji kwa nchi za kiafrika unakuwepo tu pale mirija yao inapo kuwa salama, lkn mirija ikikatwa lazima watakuchukia na watapambana kukuchafua.
kamwe usitetereke hapo ndipo kipimo cha uzalendo wako kinafanyika.

3. Tanzania hatutaki Diplomasia yakuwa wapole na kukubali kunyonywa rasilimali zetu huku wakitupumbaza kwa kutusifia sifa kemkem, hapana!! kamwe tusikubali kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.
lazima tuwe wakali inapo bidi.

Wizara ya Mambo ya nje kwa sasa imepata mwana Diplomasia nguli, Mama Mulamula, sasa tunaamini tumepata, msemaji, mkanushaji na msawazishaji wa kimataifa

4.Tunamuomba Mama Samia ktk kusimamia Rasilimali na Maslahi ya watanzania ni bora uchukiwe na wanyonyaji/mabeberu kwa ajili ya watanzania.

Endapo wasaidizi wa Mhe. Rais kuanzia na; PM, Mawaziri, makatibu wakuu, ma Rasi, Ma Dasi, Wakurugenzi, watendaji wa vijiji na kata pamoja na watendaji na viongozi wote wa Idara za Serikali watafanya kazi zao kwa bidii, uadilifu na kujituma usiku na mchana basi kwa kufanya hivyo sio tu watakuwa wamemsaidia kupeleka maendeleo ya wana chi mbele bali pia watakuwa wame changia kulinda afya ya Mhe. Rais na kinyume chake watakuwa wamechangia kuzorotesha afya yake.
tufanye kazi kwa bidii na kwa kutumia maarifa, tuache wizi, rushhwa na ubadhirifu wa mali za umma.
 
U Ugonjwa huu siyo hatari kama inavyodaiwa! Kati ya wanaopata corona, ni asilimia ndogo Sana wanaofariki.
Magonjwa mengine asilimia kubwa ya wanaougua hufariki eg kansa!
 
Post nzuri sana! Ubarikiwe!
 
Si tuliaminishwa na tukaamini ATCL inaendeshwa kwa faida hata wakati kulikuwa hakuna wageni wengi kutokana na international flights kusitisha safari zao kutokana na corona na kwamba hata idadi ya watalii ilikuwa bado iko juu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…