Huo ni mtazamo wa Gazetti la The Economist, hata raia wanaojielewa ninaamini wana mtazamo huo huo pia.
Katika kitu natamani ndugu mwandishi, siku moja uje kuanzisha thread kuichambua
REPORT YA CAG ya mwaka huu bila kuwa biased kwa kusaka uteuzi. Bwana mkubwa hayupo nasi tena. Cha kusikitisha bungeni hayupo
Zitto wa kuichambua vizuri hio report.
Key points;
1) ATCL kuendeshwa kwa hasara ya Billion 60 tokea 2016 - 2021.
Au ndio tuseme CAG pengine ana mhujumu Marehemu Rais Magufuli
alietuaminisha kwa nguvu kubwa sana kwamba shirika linafanya kazi kwa faida, kufikia hatua shirika kupewa tuzo ya usafiri bora wa mwaka kuliko Turkey Airlines na serikali kupewa
Hundi Ya Gawio La Faida na shirika???
Na je, Rais Magufuli angekua hai, angepewa hii hii report ya CAG yenye kulikosoa shirika la ATCL na TTCL, au kuna report nyingine iliopo kwenye makabati yenye mahesabu yaliopikwa ndio angepewa kumtukuza na kutuficha raia???
2) Matumizi ya hela nyingi zilizokua zinapelekwa Wizara Ya TAMISEMI na kutokujulikana matumizi yake, kufikia Rais Samia kumsimanga Waziri Selemani Jafo wazi wazi mbele ya vyombo vya habari, na kumtaka awasilishe mahesabu ya Wizara yake ndani ya muda mfupi, ila kabla hata ya Waziri Jafo ya kuwasilisha hayo mahesabu alioamrishwa na Rais, Rais akaamua kumhamisha Wizara baada ya Siku Mbili (Pengine baada ya kujua kwamba mahesabu hayo akipelekewa hata ridhika nayo kabisa).
3) TPA kukoroga mambo kwenye matumizi ya hela (Kwa viashiria vya ufisadi uliokithiri) mpaka kufikia hatua Rais Samia kumsimamisha kazi Mkurugenzi TPA na TAKUKURU kumshikilia na kufanya upelelezi wa Mabillioni kupotea kwenye account za TPA (Za BOT na NMB).
4) Matumizi ya hela HAZINA kuchotwa hovyo na wachache kwa kigezo cha matumizi (Matumizi yasio na mashiko wala sababu wala kujulikana). Kupelekea Rais Samia kumpa maelekezo CAG afanye ukaguzi upya wa matumizi ya hela zilizotoka hazina kuanzia January 2021 - March 2021.
5) Mikopo mingi sana kuchukuliwa na serikali kimya kimya bila kupitia bungeni, mikopo hio ya kimya kimya mingine bila hata kupitia katika Account za serikali na hela kuwa deposited kwenye Account za contractors na wauzaji wa ndege. Kitu kilicho sababishia serikali kuwa na deni zaidi kwa ukubwa ndani ya miaka 5 kuliko miaka 10 ya Kikwete.
Rais Samia kifupi, ana mashaka makubwa na matumizi ya hazina kuanzia mwaka huu kuanza (Ni aibu kwa watendaji kumfanya Rais awe ana mashaka na taasisi zao) na ana mashaka makubwa hasa na TPA.
Tulikua tunaaminishwa katika utawala ya 2015 - 2021 kulikua hakuna ufisadi kabisa, na mafisadi walikomeshwa kisawasawa sambamba na kutothubutu kuifisadi nchi. Raia walifurahi na kushangilia sana kwa hilo kwani mpambanaji wa mafisadi hatimae alipatikana kuwatetea wanyonge.
Ila katika hali ya kushangaza, na haya yaliotokea hivi karibuni kuna sintofahamu na imani imeanza kubadilika kabisa, kwamba ufisadi ulikuwepo ila
"VITISHO VYA KUOGOPA KUIKOSOA NA KUIHOJI SERIKALI YA AWAMU YA 5" ndio sababu ya raia kuaminishwa kwamba hakuna ufisadi na mengineyo, ila sasa raia wanaanza kuamini ufisadi ulikuwepo kama awamu zilizopita (Na wengine wakiamini ufisadi umezidi awamu zilizopita - tuvute subira).
Na sisi wengine tunaamini, waliokua wanapata taarifa za ufisadi (Hasa waandishi wa habari wa kipelelezi) walikua wakiogopa sana kuweka wazi taarifa hizo, kwa kuhofia kupotezwa kama kina Azory Gwanda au kupewa kesi za uhujumu uchumi. Kasoro waandishi mliokua mnasaka uteuzi kwa kusifia hata yasio sifika.
NOTE THAT: baada ya awamu ya 6 kuingia madarakani, ndani ya week moja tu baadhi ya magazeti (Mfano Raia Mwema) wameanza kuisaidia serikali kutoa taarifa za ufisadi unaofanyika katika taasisi za serikali, kama hela zilizotolewa hazina kuanzia January 2021 mpaka March 2021 kwa kuweka wazi mpaka Account Number za benki na kiasi cha pesa zilizokua zikitolewa bila maelezo.
Issue ya Makontena Ya Makinikia, imeanza kuchukua taswira mpya, leak zimeanza kusambaa kwamba tume ya Prof fulani baada ya kufanya uchunguzi, ili baini kwenye makontena ya mchanga ule katika kila kontena la 20Ft kulikua na 0.7% ya dhahabu na sio 7.0% kama walivyolazimishwa kuandika kwenye report na Marehemu Boss Kazi baada ya kuona alikurupuka kwenye maamuzi (For the sake of political sympathy and legal consequences).
Acacia, mtoto wa ndani ya ndoa ya Barrick alikua akilipia kodi ya 0.7% ya dhahabu katika kila kontena la 20Ft kama ilivyotakiwa kisheria, na baada ya Boss Kazi kukurupuka na kufanya maamuzi bila kujiridhisha kwa kuunda tume ya uchunguzi aliamua kuyazuia makontena yale, report ilivyotoka ya tume ilibidi data kugeuzwa na kupikwa kuwa 7.0% ya dhahabu katika kila kontena badala ya 0.7%, Acacia ndio wakakutwa wanakwepa kodi.
Tulisubiri sana, zile NOAH moja kwa kila Raia kutoka kwa Acacia, ila kimya kilitanda mpaka umauti ukamfika alietupa ahadi ile. Tuliogopa ku hoji kipindi cha uhai wake, kwani tulimzoea kwamba hapendi kubanwa kwenye kona kwa hoja zenye mashiko. Pia tulimzoea alivokua akimaanisha pindi anaongea kwa kutumia maneno kuhusiana na serikali ya awamu ya tano
SERIKALI YANGU, MIMI NINATAKA, tofauti na Mama anavyotumia maneno hayo na jinsi alivyoyabadilisha
SERIKALI YETU, SISI TUNATAKA.