Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Rais Samia Suluhu Hassan, jana usiku alishiriki katika uzinduzi wa Global Africa Investment Summit (GAIS) uliofanyika jijini Dubai, hatua inayolenga kuimarisha nafasi ya Afrika katika kuvutia uwekezaji wa kimataifa unaozingatia uhalisia wa kifedha na mipango ya muda mrefu.
Akihutubia mkutano huo, Rais Samia alisema kuwa wawekezaji wa kimataifa hawatafuti fursa pekee, bali wanahitaji mazingira yenye uaminifu, ikiwemo uthabiti wa sera, taasisi imara na serikali zinazotekeleza ahadi zake.
Alibainisha kuwa Tanzania imechukua hatua za kimkakati kuboresha mazingira ya uwekezaji kupitia uwekezaji mkubwa katika sekta ya nishati, reli, bandari na miundombinu ya uchukuzi.