GE2025 Samia: Tumejipanga kulinda nchi hii wala hakutakuwa na vurugu siku ya uchaguzi

GE2025 Samia: Tumejipanga kulinda nchi hii wala hakutakuwa na vurugu siku ya uchaguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mgombea wa Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa akiwa Kama Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama amejipanga kuilinda Nchi hii na hakutakuwa na vurugu zozote wala chochote na kuwataka wananchi waende kupiga kura siku ya uchaguzi na kurudi Nyumbani.
 
20250920_165230.jpg
20250920_165551.jpg
 
Mgombea wa Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa akiwa Kama Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama amejipanga kuilinda Nchi hii na hakutakuwa na vurugu zozote wala chochote na kuwataka wananchi waende kupiga kura siku ya uchaguzi na kurudi Nyumbani.
Mmejipanga "nchi hii" kufanya uhalifu?

Huu ni wakati sahihi kabisa kwa waTanzania kuwashughulikia majambazi wasiendelee kuleta madhara kwa nchi yetu.
Hapajawahi kuwepo na fursa nzuri kwa waTanzania kama hii ya kuwavurumisha majambazi hawa.

Jambazi yeyote hutishia kwa silaha; huyu hana tofauti na hayo mengine. Ni lazima yanyang'anywe hizo silaha na kuyashughulikia moja kwa moja.
WaTanzania wasipofanya hivyo wakati huu, maana yake ni kwamba majambazi wamepewa nafasi nyingine ya kuendelea kuzitumia hizo silaha kuwanyanyasa.

Mtanzania, kataa kutumiwa na haya majambazi. Usiende kupiga kura; hakuna polisi atakayekufuata nyumbani kwako kwa mtutu wa bunduki kukupeleka kituoni kupiga kura.
Bora zaidi; jitokeze, ungana na waTanzania wenzako kuzuia haramu hii wanayoitumia kuhalalisha ujambazi wao. Nenda kashiriki kuzuia uchafuzi.
 
Halindi nchi, analinda ulaji wake na genge lake.

Wana CCM wanaposema tutalinda amani kwa wivu mkubwa, wanamaanisha amani ya mioyo yao, amani ya wao kuendelea kutawala.
 
Unalinda maslahi yake kwa kivuli cha nchi na amani
 
Jeshi la nchi lipo kwa kulinda watawala tu lakini kihalisia jeshi linatakiwa liweze kuilinda nchi. Jee hili jeshi lipo imara kuzuwia uvamizi wa nchi nyengine hapa nchini?.
 
Mgombea wa Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa akiwa Kama Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama amejipanga kuilinda Nchi hii na hakutakuwa na vurugu zozote wala chochote na kuwataka wananchi waende kupiga kura siku ya uchaguzi na kurudi Nyumbani.
Hata Nepal walikuwa na amiri wao
 
Back
Top Bottom