Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Akiomba kura kwa wagombea wa nafasi za udiwani na ubunge kwenye majimbo na Kata za Mkoa wa Rukwa leo Jumapili Oktoba 19, 2025, mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Samia Suluhu Hassan amewaomba wananchi kuwachagua wagombea hao na kutowachanganya na wengine, ili iwe rahisi kuwasimamia na kuwawajibisha watakaoshindwa kutimiza majukumu yao.
Akizungumza na wananchi na wanachama wa chama hicho Mjini Sumbawanga, akihitimisha mikutano ya kampeni mkoani Rukwa, Samia amesema: "Kama mmeshapitiwa pitiwa huko na kusema katika kata hii msimpe huyu wa kijani, mpeni wa rangi hii, mtakuwa mnajichelewesha kwa sababu mkiwachanganya hawa madiwani wataenda kubishana kuwa mradi uende hapa wengine wanasema hapana."
Mtakuwa mnajichelewesha kwa maendeleo, niwaombe sana kachagueni madiwani hawa niliowaleteeni kutoka Chama cha Mapinduzi, hawa lugha yao ni moja akitokea mmoja ama wawili kati yao wanafanya ukorofi, chama kitasimama kuwaadabisha, wakifanya ukorofi wa vyama vingine chama chetu hakiwezi kuwaadabisha, hatutaweza na huo ukorofi utaendelea kwa miaka mitano ya baraza la madiwani,”amesema Samia.