Sampuli ya wachimbaji wachache waliofanya kufufu ya kuchezea noti ndio sababu ya kuwanyima ruzuku mamilioni ya Watanganyika wanaohangaika maporini?

Labda sikumsikiliza mpaka mwisho yule Rais wa wachimba madini, Hivi kuna sehemu yoyote kwenye hotuba yake aliomba ruzuku ya Serikali kwa wachimbaji Madini? Kama nilimuelewa vizuri Rais wa vito na madini aliomba wachimbaji wapate nafasi ya kusafiri na Vasco Dagama kwenye ujumbe wake anapokwenda nje ya nchi na dege kubwa la Jamuhuri. Lakini aliomba soko la Dubai lihamishiwe Tanzania ili madini yauziwe hapa hapa.
 
Badala waseme hawana hela wanasingizia ya Katoro
 
Bila kuingilia Siasani; Ukweli japokuwa ni mchungu, kwenye sekta ya madini wachimbaji wadogo wakipata (wenyewe wanaita shimo limetema au wamepasua chungu)huwa wanaonesha vituko sana kwa namna wanavyotumia Fedha walizopata kwa kuyauza madini yao. Ipo mifano yao mingi e.g. Yule askofu wa mererani aliyekuwa anagawa fedha, kule Ludewa (sikumbuki mwaka) walikuwepo wachimbaji wa dhahabu kule Mavanga waliokuwa wakipata pesa kwa kuuza "vikole" wanaogea pombe maarufu kipindi hicho iliyoitwa stela atoir au wanafunga vilabu vya pombe(Ulanzi) n.k.n.k......
 
Hao wachimbaji ndiyo wanaleta pesa za kununulia madawa.
 
Mnahitaji uthibitisho gani zaidi kuwa huyo mazeri ni haramu ndani na nje?
 
Hao wachimbaji ndiyo wanaleta pesa za kununulia madawa.
muhimu kujua mchango wao kwenye pato la taifa ni kiasi gani na why wao tena wapewe ruzuku badala ya kutumia financial institutions kupata financing

Biashara sip NGO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…