Samsung na LG kutowauzia display HUAWEI

Samsung na LG kutowauzia display HUAWEI

Almendezz

Senior Member
Joined
Aug 17, 2020
Posts
160
Reaction score
405
Tarehe ya mwisho ya Septemba 15 inaonekana inazidi kutisha kwa Huawei - laini ya usambazaji ya kampuni hiyo itapungua pamoja na kukatwa kutoka kwa supplier wa chip wa TSMC. Reuters inaripoti (ikinukuu media ya Kikorea) kwamba Samsung Display na LG Display zinatarajiwa kusitisha uuzaji kwa kampuni hiyo ya simu, kwa sababu ya kukazwa kwa vizuizi vya biashara kutoka Amerika.

Chips zinazotumika katika display zinaarifiwa kuathiriwa na vikwazo vya Amerika, ndio sababu ya kusimamisha biashara. Chosun Biz, ambaye alitoa habari hiyo, anataja vyanzo vya industry akisema kwamba Huawei sio sehemu kubwa ya ununuzi kutoka kwa wazalishaji wote hao wa display.

Walakini, kampuni hizo mbili za Kikorea ni wasambazaji muhimu kwa Huawei. Kampuni hiyo imeweza kutofautisha na itatoa display yote ya Huawei Mate 40 kutoka BOE, hata hivyo Mate 40 Pro itatumia mchanganyiko wa display ya BOE, Samsung na LG.

Wakati viwanda nchini China haviwezi (bado) kutengeneza chips za nm 7 na 5 nm kwa matumizi katika flagship zijazo, usambazaji thabiti wa display unapaswa kuwa rahisi kupata ndani - BOE inaweza kuongeza uzalishaji na ikiwa sivyo, CSOT na Visionox pia zinafanya kazi kwenye display ya on-cell OLED.

Uonyesho wa LG unasema kuwa hii itakuwa na athari ndogo kwa mauzo yake na kwamba itawashawishi wateja wake kwenda mbele. Samsung Display haikutoa maoni juu ya hali hiyo.

Je ni nani anayeathirika zaidi kwenye hili?
China, marekani, huawei, samsung au LG??
 
Huawei si kampuni kubwa in electronics science , inashindwa kutengeneza display

Ni kweli unachosema lakini nnachoamini mimi ni ngumu sana kuweza kujitosheleza kwa asilimia 100 katika production line. Lakini simaanishi kwamba haiwezekani
 
Kwahiyo some parts wanaagizakutoka kwa wengine! Nimejiuliza sana kuwa hawa si magwiji wa electronics, sasa hawana TECHNOLOGY ya kutengeneza display?
 
Exactly wengi wanategemeana.

Mfano Apple anatumia display za samsung, sony pamoja ni mzoefu wa muda mrefu kwenye camera lakini anatumia camera lens za samsung katika baadhi ya simu zake.

Kifupi unaweza kujiuliza vp mfano LG anamtengenezea display HUAWEI lakini huawei ana simu bora kulinganisha na LG. HAPO ndo kunakuja kitu kinaitwa OEM na ODM mkuu
 
Huawei si kampuni kubwa in electronics science , inashindwa kutengeneza display
Kwenye Technology hamna mtu anayejitegenea asilimia mia kwa resources na technology kuna kutegemeana hata samsung mwenyewe hizo display anazozitengeneza anategemea baadhi ya vitu kutoka Japan ndo maana ukifuatilia mgogoro wa South Korea na Japan Samsung alikua na hofu sana maana ungeathiri utengenezaji wa display zake.
 
Kwahiyo some parts wanaagizakutoka kwa wengine! Nimejiuliza sana kuwa hawa si magwiji wa electronics, sasa hawana TECHNOLOGY ya kutengeneza display?

Kwan unavoona simu za samsung wametengeneza kila kitu?
 
Kwahiyo some parts wanaagizakutoka kwa wengine! Nimejiuliza sana kuwa hawa si magwiji wa electronics, sasa hawana TECHNOLOGY ya kutengeneza display?

Kwenye technology kuna kitu kinaitwa OEM . yaani hakuna kampuni inayotengeneza bidhaa za computer na vifaa vyake.

Angalia kwa mfano Dell:
Processor -intel
Hdd -seagate
Ram- Hynix
Display - Phillips

Hata vifaa vya electronics,
Unakuta TV ya LG, ndani kuna chip ya samsung , toshiba etc.
 
Processor -intel...
ASANTE SANA KWA ELIMU!

Swali tena: Does that mean kuwa hawana technology ya kutengenza hivyo vitu? Wakiamua kuweka kiwanda cha display hawawezi kwa vile they do not have that technical know-how?
 
Kuna suala la intellectual property kuna suala la Gharama na suala la ubora control n.k

Samsung mpaka Leo anatumia Android ya google, anategemea apps za makampuni mengine Kama Facebook n.k Leo hii huwezi sema ngoja nitengeneze kila kitu changu utaishia kuingia gharama kubwa na utafeli biashara.

Kama unauza juice na unapata maji ya bakhressa Kwa Bei ndogo haina haja ya kutengeneza maji yako. Kila mtu afanye kazi yake. Hii ni sababu mojayapo Apple amefanikiwa sana kibiashara.
 
Nimekupata vema! sasa wakikataa kumpa display si Huawei inakufa. Basi ubabe ubabe unaanza kutengeneza kila kitu ingawa it might take years
 
Unatengeneza kila kitu kivipi? Nimetoa mfano wa software Leo fb waondoe social media zao (Whatsap, insta na fb) kwenye simu za huawei au zisiruhusiwe unadhani huawei ataweza kutengeneza social media zake ? Unafikiri kuna mtu atanunua huawei? Kuna vitu vingine lazima utegemee watu, kutengeneza display inaweza isiwe issue lakini je itakulipa? Investment inaweza kuwa kubwa huku unauza simu chache ukala hasara. Ni Kama lile suala la kuchenjua mchanga wa dhahabu Kama una kiasi kidogo huwezi kuweka smelta ni bora upeleke Kwa mtu mmoja afanye hiyo kazi . Ni suala la cost and benefits

Au tuseme Muuza chips akisema alime viazi, alime alizeti akamue mafuta, awe na kiwanda cha kutengeneza majiko, achome mkaa na afuge kuku, awe na kiwanda cha vijiko na uma na vijiti, alime nyanya na vitunguu, alime matangoKwa ajiri ya salad , awe na kiwanda cha chumvi n.k

Unafikiri atafanya biashara au atakuwa anapoteza muda ??
 
😂 😂 😂 😂 mfano murua kabisa
 
Kwahiyo some parts wanaagizakutoka kwa wengine! Nimejiuliza sana kuwa hawa si magwiji wa electronics, sasa hawana TECHNOLOGY ya kutengeneza display?
Hakuna kampuni inayojitosheleza kwa kila kitu
 
Kwahiyo some parts wanaagizakutoka kwa wengine! Nimejiuliza sana kuwa hawa si magwiji wa electronics, sasa hawana TECHNOLOGY ya kutengeneza display?
iPhone wenyewe kuna chip kama memory na baadhi ya chip wanatumia za Samsung, Sundisk Toshiba. Kama iPhone 11 ina chip memory za Sundisk na Samsung
 
Kwenye technology kuna kitu kinaitwa OEM . yaani hakuna kampuni inayotengeneza bidhaa za computer na vifaa vyake.

Angalia kwa mfano Dell:
Processor -intel
Hdd -seagate
Ram- Hynix
Display - Phillips

Hata vifaa vya electronics,
Unakuta TV ya LG, ndani kuna chip ya samsung , toshiba etc.
Kweli kabisa ndivyo ilivyo
 
Unatengeneza kila kitu kivipi? Nimetoa mfano wa software Leo fb waondoe social media zao (Whatsap, insta na fb) kwenye simu za huawei au zisiruhusiwe unadhani huawei ataweza kutengeneza social media zake ? Unafikiri kuna mtu atanunua huawei? Kuna vitu vingine lazima utegemee watu, kutengeneza display inaweza isiwe issue lakini je itakulipa? Investment inaweza kuwa kubwa huku unauza simu chache ukala hasara. Ni Kama lile suala la kuchenjua mchanga wa dhahabu Kama una kiasi kidogo huwezi kuweka smelta ni bora upeleke Kwa mtu mmoja afanye hiyo kazi . Ni suala la cost and benefits

Au tuseme Muuza chips akisema alime viazi, alime alizeti akamue mafuta, awe na kiwanda cha kutengeneza majiko, achome mkaa na afuge kuku, awe na kiwanda cha vijiko na uma na vijiti, alime nyanya na vitunguu, alime matangoKwa ajiri ya salad , awe na kiwanda cha chumvi n.k

Unafikiri atafanya biashara au atakuwa anapoteza muda ??
Mkuu kwa mifano uliyo toa kama hakuna alie elewa usijichoshe mkuu.
 
Back
Top Bottom