Samsung yazidi kuwa Iphone

Samsung yazidi kuwa Iphone

Mimi ni Sony fan hadi watapofunga kiwanda 😀!
Sahizi niko na XZ1 nainjoy unyama tu juzi nimesahau bomba maji yamejaa hadi chumbani cha ajabu simu iko kwenye maji ila haijaharibika. Kumbe kitu ni waterproof bana 😀 😀 😀
Sony fan too
 
Uache samsung uende wapi?
Iphone?
Google?
Au wapi?
 

Samsung Galaxy Note20 Ultra 5G, the best one😘​

Nishawai kumiliki galaxy note 8 mkuu ilikua inachemka sana yani inapata moto hatari. je hizi note 10+ na 20 hazina shida hiyo nataka nivute moja.
 
Watu huwa mnadhani simu ni Samsung, iPhone na Google Pixel tu. Mnasahau kuna Xiaomi, Oppo, vivo, One Plus, Sony, Realme, Nothing phone nk
Hao wachina unajitahidi kuwapigia promo lakini wapi, soko hasa la Africa haliwaelewi
 
Mimi ni mpenzi mkubwa Sana wa simu za android na simu yangu pendwa ni Samsung lakini huku tunakoelekea naona kabisa nitaisaliti chama.Sababu ni kuwa Samsung wanaiga vitu vingi Sana ambavyo havina msingi kutoka Kwa kampuni ya simu ya Iphone.

Hivi ni vitu baadhi ambavyo Samsung kaiga kutoka Kwa Iphone na vimeleta mabadiliko hasi Sana kwa watumiaji wa hizi simu za Samsung;


1 Wameiga kuondoa 3.5 mm jack kutoka kwenye simu za Iphone ;

Mwaka 2017 iphone waliondoa 3.5mm jack ya kuingiza Ear phones kutoka kwenye simu zao za Iphone 7. Matokeo yake Iphone walipondwa Sana na watumiaji wake na kukemewa vikali na kupondwa na makampuni ya simu ikiwemo Samsung.Chanzo Cha kuondoa 3.5 mm jack ilikuwa ni sababu Iphone walishindwa kutengeneza kioo full screen huku 3.5mm Jack ikiwepo.Iphone wanadai kwamba waliondoa 3.5 mm jack Ili waweze kutengeneza full screen BIla kizuizi.Kitu ambacho simu za android ilishaweza kutengeneza huku 3.5 mm jack ikiwepo.Tuseme tu android phones ZIPO mbele kiteknlolojia zaidi ya iPhone .

Swali langu ninajiuliza kwanini Samsung waliamua kuondoa 3.5 mm jack kwenye simu zao Kwa kumuiga iPhone wakati wanajua Iphone waliondoa hicho kitu sababu ya kukosa teknolojia ya kutengeneza full screen BIla kutoa 3.5mm jack?

2 Wameiga kutoweka charger na cover za simu kwenye Box la Simu mpya kama wanavyofanya Iphone ;

Nasikitika Sana kuona Samsung wamepata ujasiri wa kupakia simu tu kwenye Box BIla charger Wala Cover kama simu zingine za Android zinavyofanya.Watu wanatoa mamilioni lakini hawapati product zilizokamilika kwenye Box.Ni upuuzi mtupu.


Wakati simu zingine za Android zinajitahidi kuweka Hadi pre installed screen protector na accessories za simu zinazohitajika Sana Samsung wapo busy wanazidi kuziondoa.


Mimi ni mdau wa Samsung lakini hapa niseme tu Samsung wamefeli pakubwa.

Ni ajabu kukuta Flagship phone kama galaxy S23 ultra imekuja tu na USB Haina charger ni upuuzi mtupu tu.

NI BORA NIHAMIE KAMPUNI ZINGINE ZA SIMU MAANA SAMSUNG WAMEBADILIKA KUWA IPHONE SIO WAO TENA.

Shame on you ShameSung
Dah,
Sasa hili bandiko hapa JF wataliona?!
 
Hao wachina unajitahidi kuwapigia promo lakini wapi, soko hasa la Africa haliwaelewi
Tatizo la soko la Africa ni MA Agent, hakuna kampuni yoyote ambayo official kabisa ipo hapa kwetu bali ni Agents wanaochukua hizo Tenda.

Vivo, Oppo, Xiaomi wote wapo ila ukienda maduka yao bei wanazo uza balaa, halafu models wanazoleta sio zile ambazo zinafanya hizo brand kujulikana worldwide.

Kama Vivo Tanzania simu nyingi za bei rahisi hazina value kivile na ukikuta simu nzuri (kama Vivo V30) bei inazidi milioni moja. Mtu unaona bora uagizishie online ama ununue Samsung.
 
Haya makampuni makubwa yanaangalia soko la ulaya na uarabuni wanataka nini maana ndio wenye pesa...
Sasa wewe mnunua second hand huwezi kuwa na thamani.
Tumia kilichopo sio unachotaka
 
Hao wachina unajitahidi kuwapigia promo lakini wapi, soko hasa la Africa haliwaelewi
Makampuni ya Kichina yenyewe mengi interest yao ni India na nchi nyingine za Asia kuliko Africa. Huku wachina wenye interest na sisi ni Tecno na Infinix ndio wameshika soko. Sioni ubaya kwenye hiyo post yangu mpaka usema napiga promo. Sony imebase Japan na Nothing phone imebase England ila wewe umeona Wachina tu. Tena hasa hasa umeiona Xiaomi hapo ndo ukakimbilia kuponda
 
Nishawai kumiliki galaxy note 8 mkuu ilikua inachemka sana yani inapata moto hatari. je hizi note 10+ na 20 hazina shida hiyo nataka nivute moja.
Hizo used mkuu mpya hutapata kokote
 
Back
Top Bottom