Mkuu itoshe tu kusema umekuwa brainwashed na propaganda za kibiashara za kihuni za makampuni ya simu
Unapata wapi ujasiri wa kutetea ujinga kama huo wa uchafuzi wa mazingira?
Ukweli ni kwamba Apple waliopata mabilion ya dola kwa kuuza accessories baada ya kuzitoa kwenye box
Hii ndio sababu kuu na sio ujinga wa uchafuzi wa mzingira
Jamaa yangu alinunua S23 utra hadi leo hii amebadili kwa kununua charger zaidi ya 5 kwasababu kila charger aliyonunua au kuagiza online zilikuja kugoma kuchaji baadae
Hivi kweli uchukue chaja ya Samsung yako ya mwaka 2017 uanze kuchajia simu ya 2023?
Au unadhani kila charger inayoingia kwenye simu basi inafaa kuchajia?
Jiulize kwanini kila toleo linatoka na charger yake tena zinautofauti?
Mimi binafsi nina charger zaidi ya 20 za iPhone zilizo kufa kwenye store yangu ya makabrasha ghafi kwasababu kila charger ninayo nunua haimalizi mwaka inakufa
Lakini ningewekewa charger original kwenye box uhakika miaka 5 na zaidi