Samsung yazidi kuwa Iphone

Mimi ni Sony fan hadi watapofunga kiwanda 😀!
Sahizi niko na XZ1 nainjoy unyama tu juzi nimesahau bomba maji yamejaa hadi chumbani cha ajabu simu iko kwenye maji ila haijaharibika. Kumbe kitu ni waterproof bana 😀 😀 😀
Sony fan too
 
Uache samsung uende wapi?
Iphone?
Google?
Au wapi?
 

Samsung Galaxy Note20 Ultra 5G, the best one😘​

Nishawai kumiliki galaxy note 8 mkuu ilikua inachemka sana yani inapata moto hatari. je hizi note 10+ na 20 hazina shida hiyo nataka nivute moja.
 
Watu huwa mnadhani simu ni Samsung, iPhone na Google Pixel tu. Mnasahau kuna Xiaomi, Oppo, vivo, One Plus, Sony, Realme, Nothing phone nk
Hao wachina unajitahidi kuwapigia promo lakini wapi, soko hasa la Africa haliwaelewi
 
Dah,
Sasa hili bandiko hapa JF wataliona?!
 
Hao wachina unajitahidi kuwapigia promo lakini wapi, soko hasa la Africa haliwaelewi
Tatizo la soko la Africa ni MA Agent, hakuna kampuni yoyote ambayo official kabisa ipo hapa kwetu bali ni Agents wanaochukua hizo Tenda.

Vivo, Oppo, Xiaomi wote wapo ila ukienda maduka yao bei wanazo uza balaa, halafu models wanazoleta sio zile ambazo zinafanya hizo brand kujulikana worldwide.

Kama Vivo Tanzania simu nyingi za bei rahisi hazina value kivile na ukikuta simu nzuri (kama Vivo V30) bei inazidi milioni moja. Mtu unaona bora uagizishie online ama ununue Samsung.
 
Haya makampuni makubwa yanaangalia soko la ulaya na uarabuni wanataka nini maana ndio wenye pesa...
Sasa wewe mnunua second hand huwezi kuwa na thamani.
Tumia kilichopo sio unachotaka
 
Hao wachina unajitahidi kuwapigia promo lakini wapi, soko hasa la Africa haliwaelewi
Makampuni ya Kichina yenyewe mengi interest yao ni India na nchi nyingine za Asia kuliko Africa. Huku wachina wenye interest na sisi ni Tecno na Infinix ndio wameshika soko. Sioni ubaya kwenye hiyo post yangu mpaka usema napiga promo. Sony imebase Japan na Nothing phone imebase England ila wewe umeona Wachina tu. Tena hasa hasa umeiona Xiaomi hapo ndo ukakimbilia kuponda
 
Nishawai kumiliki galaxy note 8 mkuu ilikua inachemka sana yani inapata moto hatari. je hizi note 10+ na 20 hazina shida hiyo nataka nivute moja.
Hizo used mkuu mpya hutapata kokote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…