Samsung yazidi kuwa Iphone

Charger ya Sony Xperia 1 IV (30W) inauzwa kwa £50 according to gsmarena.com
Hii bei ni kubwa kwa kitu kama charger
 
Hizo accessories unazoziongelea ni rahisi kupata labda za TECNO na Infinix ambazo ni za Oraimo.Lakini Accessories za Samsung na Iphone hazipatikani kirahisi na zikipatikana unakuta nyingi sio Original na ukikuta ni Original unakuta ni gharama Sana.Na unakuta hawakuwekei charger makusudi Ili wakupige Hela waingize Faida ukinunua charger separate, ngoja tuendelee kukomaa na One plus au Xiaomi.
 
Sio kweli, Samsung accessories zake zimezagaa madukani sana.

Na sio lazima iwe kampuni ya Samsung tu, unaweza pata charger original safi na isiwe Samsung na ukaitumia fresh tu.

Product original hauwezi kuuziwa bei sawa na replica, hata hivyo charger type C Original haizidi 15K
 
Hiyo sony ni poor design, a phone from the past, 2015 design in 2023
Hii design sio ya 2015
Hata hivyo ni identity ya simu za Sony.
Wanatengeneza simu zenye 21:9 aspect ratio ambayo hutumika katika muvi nyingi. Sony wanasema kuwa zaidi ya 70% ya movies zilizopo Netflix zina aspect ratio ya 21:9. Kwa hiyo ukitumia hizi simu mpya za Sony kuangalia muvi yenye 21:9 ile movie itajaa kwenye screen yote bila kuacha nafasi au kuform black strips. Ndio maana simu zao zinaonekana ndefu na nyembamba kuliko simu nyingine.

Sony ipo kwa ajili ya movie fans ndio maana anaweka pixel density kubwa kwenye simu zake kuliko wapinzani mfano hiyo Xperia 1 IV ina 643ppi. Lengo ni kufanya uone details clearly ukiwa unaangalia movies.
Simu zao ni miongoni mwa simu zenye speakers bora sana tena kama hii Xperia 1 IV ina hadi base ya kutosha. Hii inaweza kuwafaa wapenzi wa mziki ila speaker Bora ni muhimu sana kwa wadau wa movie
Display ya Sony Xperia 1 IV inaweza kuswitch to 4K resolution ikiigundua tu unaplay video. Wakati hii inasababisha ulaji mkubwa wa chaji lakini lengo ni kukupa top notch experience ukiwa unaangalia movies

Bado anaweka microSD card slot ili uweze kuhifadhi movies kwenye memory card. Anakupa hadi uhuru wa kutumia 3.5mm jack ili uweze kusikiliza sauti ya kwenye movies kwa kutumia wired earphones

Ikiwa Sony imeweza kufanya mambo yote hayo ili tu ufaidi kuangalia movies basi hakuona shida kuchange aspect ratio pia ili iendane na ile ya kwenye movies. Ndio hiyo design unayoiona. Hakutaka kutumia kamera ya katikati ndani ya display area ili asipunguze nafasi ya kuangalia video/movies na wanaamini simu zao ndio Bora zaidi kwa kuangalia movies

Hiyo design inawafaa Sana wanaopenda kuangalia movies kwenye simu. Mi naona ipo poa sana
 
Yaani mkuu Hawa Sony nawapongeza Sana Wanajaribu kuwa wabunifu Kwa malengo ya kuzidi kuwapa wateja wanachokitaka na sio kuigaiga mambo mengine ambayo yanaleta karaha Kwa mtumiaji wa simu .Sasahivi watu wanaotumia airpods Wana disadvantage ya kutakiwa kuzicharge Kila muda .
 
pixel alishaanza kitambo kutokuweka hiyo 3.5
 
Sasahv napata tabu sana linapokuja suala la earphones. Nilinunua zile za Bluetooth bei chee case yake ikafa, nikanunua za waya type C na nilizitunza kwelikweli ghafla zikaanza kupiga sikio moja nazo zikafa. Na napenda za waya kuliko hizo za bluetooth.
 
Accessory genuine inayokuja na simu ni tofauti na hizi za kuokota Kkoo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…