Samwel Sita, speaker mtarajiwa bunge la katiba

Msingida

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
10,239
Reaction score
11,731
Wanajamvi,
Nimesoma na kusikiliza vyombo mbali mbali vya habari na mitandao ya jamii, Mh.6 anaonekana kukubalika zaidi kuliko wagombea wengine kutokana msimamo wake thabiti na ile slogan yake ya "Standard and speed".
Unashauri nani kuwa speaker wa Bunge la Katiba? Tiririka
 
Tunahitaji kiranja wa bunge la katiba ambaye hana chama ili asimamie mijadala vizuri, Hii ya kutaka CCM ndo watoe wmeyekiti haina nia njema na katiba hii.

 
Bunge maalum la Katiba halina na halitakuwa na Speaker pengine unamaanisha Mwenyekiti - fanya marekebisho kwenye hoja yako
 
CCM hawatamchagua Sitta - I can bet on this!
 
Kutokana na uzoefu aliounyesha akiwa Spika nina imani anaweza kuifanya Vizuri kazi hii ya Uenyakiti wa Bunge la katiba.
pamoja na ukweli kuwa 6 ni mCCM, anajitahidi kiasi chake akiwa kwenye kiti kumantain neutrality inayotakiwa. nina imani wajumbe wanalijua hili na hivyo watafanya maamuzi sahihi wasaa utakapowadia!
 
Bunge maalum la Katiba halina na halitakuwa na Speaker pengine unamaanisha Mwenyekiti - fanya marekebisho kwenye hoja yako


Kirangeta,mazoea yana tabu.Ni m/kiti.naomba wasaidie kurekebisha heading Mods
 
Jaji mkuu mstaafu Samatta angekuwa mwenyekiti tungepata katiba ya kuheshimiwa!! Wakimpa Chenge watakuwa wameinajisi rasimu ya katiba na haitakuwa na kheri!!!
 

Indeed Sitta is the man to beat! kwa bahati mbaya kitu cha mwisho wanachotaka kukisikia wenzetu CCM ni hicho ulichokitaja; Standard and speed! kwa CCM; the ends justify the means; mizengwe mwanzo mwisho ili kulinda status quo; mtu anayeweza kusababisha MaCCM wawajibishwe hawatamkubali n'go!!

Gafulale! utasikia kanuni zimebadilishwa kwamba tunahitaji mwenyekiti awe mrefu sio chini ya futi 6 au mwanamke! hapo tayari ujue mzee wa Kasi na Viwango ameenguliwa, hawana aibu wale!

Mwenyekiti to be ni Mzee wa Vijisenti Chenge! you bet!
 
Sita kwa uenyekiti anafaa hata kama yuko CCM na atakuja na mambo mazuri na si vinginevyo.
 
wewe unaota au?

Sio kwamba ninaota CCM wanaichukulia vile vile kama sehemu ya kutafuta muafaka katika chama.

Endapo akipewa sita maana yake kambi ya Lowasa itakuwa imepigwa bao hali kadhalika akipewa Chenge kambi ya kina sitta itakuwa imepigwa bao. Hivyo basi CCM itajitahidi kumuweka mtu asiyefungamana na upande wowote na hapo ndipo Pandu Amir Kificho anabakia kuwa keti muhimu kwa CCM. Ni vyema tukakumbuka mwenyekiti wa bunge maalumu la katiba hajichagui isipokuwa ni mikakati madhubuti inayokuwa imewekwa hapo awali.
 

Mkuu nahisi watu wanaesabu nazi wewe unaesabu makumbi!
...
Haiwezekani unaloliongea kwa sababu huyo kificho kwa sasa ni mwenyeki wa muda!
 
Mkuu nahisi watu wanaesabu nazi wewe unaesabu makumbi!
...
Haiwezekani unaloliongea kwa sababu huyo kificho kwa sasa ni mwenyeki wa muda!

Ni kweli Kificho ni mwenyekiti wa muda ila ndio huyo huyo atakaye pita kama mwenyekiti wa kudumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…