Sanamu la KEMET huko Misri

Sanamu la KEMET huko Misri

Mtu yeyote anayetaka kujifunza historia ya Afrika, ni vyema akaanza kujifunza kwanza historia ya Kemet kwani hapo ndipo inapopatikana elimu, urithi, historia, ufahari wa bara letu la Afrika.

Pia tufahamu kwamba Kemet ndio eneo la kwanza ulimwenguni kuanza kustaarabika.

Unaweza ukawa unajiuliza, Kemet ni wapi? Jibu ni kwamba, KEMET ni Misri ya Kale.

Leo hii, asilimia kubwa ya raia wa misri ni waarabu, lakini huko nyuma, Misri ilikuwa ni Ardhi ya mtu mweusi. Hao waarabu walivamia misri miaka ya 639 AD ikiwa ni katika jitihada za kueneza imani ya Kiislamu.

Mojawapo ya Tamaduni za Wamisri wa kale, ilikuwa ni kujenga mapiramidi. Ingawa yapo mapiramidi mengi sana huko Misri, lakini yaliyo maarufu ni yale mapiramidi matatu yaliyoko katika mji wa Giza.

Sambamba na hayo mapiramidi Matatu, kuna kitu kinaitwa 'Sphinx'. Ni jengo lililojengwa kwa mfano wa Simba mwenye kichwa cha Binadamu. (Pichani)

Na Inaelezwa kwamba hiko kichwa ni cha Farao Khafre aliyetawala hapo kwenye miaka ya 2558 hadi 2532 BC.

Sphinx ina urefu wa takribani Mita 73 kuanzia kwenye mkia hadi kwenye viganja vya mikono. Pia urefu wa kwenda juu (kimo) ni takribani Mita 20 kuanzia kwenye Ardhi hadi kwenye utosi. Pia na upana wa Mita 19.

UNAWEZA KUONGEZEA KUHUSU SANAMU LA KEMET


.View attachment 978364


Hii elimu inakufaa wewe mwarab koko FaizaFoxy. Tulikuambia kuwa ustaarab tulianzisha sie watu weusi ukatubishia na sasa huyu mwenzako anakuja kukuelemisha ili ukawafundishe waarab koko wenzio.
 
Hivi sanamu zote zinavunjika pua tu au ni makusudi? Hahaha
aa03cbd7ad6ef1968b30b54dbeef0fd5.jpg


Sent from my SM using Tapatalk
Hahaha [emoji23][emoji23] wanatuogopa ss watu weusi balaa. BTW, black ndio race ya kwanza kuwa civilized.
 
JF huwa kuna mada nzuri sana ila zikishaingiliwa na wafia dini ndio basi tena!!
Wapo ambao huwa kazi yao ni kukashifu na kutukana dini, ni tabia ambayo nafikiri ni malezi ya nyumbani wanafundishwa chuki kila kukicha

Sent from my SM using Tapatalk
 
MKUU MBONA HATA MALAIKA NAO NI WEUSI TENA NI ILE TRAIT YA IDD AMIN DADA KABSAA
 
Huwa najiuliza sana tunaposema mtu mweusi ndie wa kwanza kustaarabika mbona maisha tunayoishi si ya kistaarabu? Ifikie point tuache kutafuta huruma ya dunia. Waliotuzidi wametuzidi tu. Kama tuliweza kuwa hivyo mwanzo iweje sasa tumekuwa kituko na watu dhalili mbele ya watu weupe ambao tuliwazidi ustaarabu awali???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi naanza kuamini kuwa wote katika mashariki ya Kati mpaka huku kwetu Afrika yawezekana tulikuwa na rangi moja kwa maana rangi ya chokleti (Hakuna mtu mwe
usi nakataa) ila Hawa wenyewe race nyeupe kama hawatupendi hivi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitu kimoja tunachotakiwa tukikubali waafrika hasa wa sub- Sahara African tulichelewa kupata civililazation ..haya mambo mengine tunaonekana kama tunaiba historia za watu ..inakuwa kama afrocentric Fantasy ..mara utasikia Yesu alikuwa mweusi,mara black walijenga pyramid ,mara jews walikuwa weusi..tatizo ni moja hatuna strong evidence za kusapport claims zetu.
Mkuu kwa nini mapiramid yapo Afrika hasa misri Sudan na Uganda na si mashariki ya kati na ulaya kama kweli hayakujengwa na watu weusi waafrika.?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom