Sanamu la KEMET huko Misri

Sanamu la KEMET huko Misri

Mtu yeyote anayetaka kujifunza historia ya Afrika, ni vyema akaanza kujifunza kwanza historia ya Kemet kwani hapo ndipo inapopatikana elimu, urithi, historia, ufahari wa bara letu la Afrika.

Pia tufahamu kwamba Kemet ndio eneo la kwanza ulimwenguni kuanza kustaarabika.

Unaweza ukawa unajiuliza, Kemet ni wapi? Jibu ni kwamba, KEMET ni Misri ya Kale.

Leo hii, asilimia kubwa ya raia wa misri ni waarabu, lakini huko nyuma, Misri ilikuwa ni Ardhi ya mtu mweusi. Hao waarabu walivamia misri miaka ya 639 AD ikiwa ni katika jitihada za kueneza imani ya Kiislamu.

Mojawapo ya Tamaduni za Wamisri wa kale, ilikuwa ni kujenga mapiramidi. Ingawa yapo mapiramidi mengi sana huko Misri, lakini yaliyo maarufu ni yale mapiramidi matatu yaliyoko katika mji wa Giza.

Sambamba na hayo mapiramidi Matatu, kuna kitu kinaitwa 'Sphinx'. Ni jengo lililojengwa kwa mfano wa Simba mwenye kichwa cha Binadamu. (Pichani)

Na Inaelezwa kwamba hiko kichwa ni cha Farao Khafre aliyetawala hapo kwenye miaka ya 2558 hadi 2532 BC.

Sphinx ina urefu wa takribani Mita 73 kuanzia kwenye mkia hadi kwenye viganja vya mikono. Pia urefu wa kwenda juu (kimo) ni takribani Mita 20 kuanzia kwenye Ardhi hadi kwenye utosi. Pia na upana wa Mita 19.

UNAWEZA KUONGEZEA KUHUSU SANAMU LA KEMET


.View attachment 978364
Sawa mkuu mwanzo mzuri
 
Back
Top Bottom