Sanamu za wanyama mzunguko (roundabout) wa Msamvu, Morogoro.

Wiki iliyopita nimepita roundabout ya Msamvu na kuona kazi nzuri ya kutengeneza sanamu zinazoonesha vivutio vyetu. Moja ya sanamu hizo ni ile ya chui akimkamata mamba. Nina tatizo na hii sanamu. Jamii ya chui wenye tabia na uwezo wa kukamata mamba wanaitwa jaguars wanaopatikana bara Amerika. Hawa wanafanana kwa muonekano na hawa chui (leopards) tulionao hapa nchini. Na jamii ya mamba ambao huweza kukamatwa/kuliwa na hawa jaguars wanaitwa caimans ambao hupatikana pia bara Amerika. Caimans wanafanana na mamba (crocodiles) hawa tulionao hapa nchini ila wao, pamoja na tofauti zingine, ni wadogo kwa umbile.

Kwa ufahamu wangu hatuna jaguars wala caimans hapa nchini. Kama hivyo ndivyo, nini mantiki ya kuweka sanamu za wanyama ambao hawapatikani hapa nchini wakati tunao wanyama wengi tu ambao tungeweza kuweka sanamu zao?
Daah huu ndiyo U great thinker, sijapata huko but this is very valid and good observations. Halafu ni ajabu sana kuweka jaguar wakati Morogoro kuna mbuga za wanyama na nature reserves nyingi tuu, pia milima ya uluguru inayotiririsha maji. Nashauri hii post ukaibandike pia kwenye ukurasa wa Mhe Kigwangala kule Twitter ataufanyia kazi, sometimes yuko sharp.
 
Natumai na 'mtaa' huu huwa anapita pita (au hata wasaidizi wake).
 
Kwani picha/sanamy zote zinazowekwa sehemu mbalimbali zipo eneo hili au hapa tz..?
Kikubwa wajmmejaribu kutengeneza tu mandhari inayovuti. Na hats wenzangu na mid tusio na uwezo hats was kwenda Mikumi National Park kuangalia wanyama basi tunapata picha.
 
Ajabu kuna watu wanakupinga na watakupinga.
Una hoja mkuu.
 
Wiki iliyopita nimepita roundabout ya Msamvu na kuona kazi nzuri ya kutengeneza sanamu zinazoonesha vivutio vyetu. Moja ya sanamu hizo ni ile ya chui akimkamata mamba. Nina tatizo na hii sanamu. Jamii ya chui wenye tabia na uwezo wa kukamata mamba wanaitwa jaguars wanaopatikana bara Amerika. Hawa wanafanana kwa muonekano na hawa chui (leopards) tulionao hapa nchini. Na jamii ya mamba ambao huweza kukamatwa/kuliwa na hawa jaguars wanaitwa caimans ambao hupatikana pia bara Amerika. Caimans wanafanana na mamba (crocodiles) hawa tulionao hapa nchini ila wao, pamoja na tofauti zingine, ni wadogo kwa umbile.

Kwa ufahamu wangu hatuna jaguars wala caimans hapa nchini. Kama hivyo ndivyo, nini mantiki ya kuweka sanamu za wanyama ambao hawapatikani hapa nchini wakati tunao wanyama wengi tu ambao tungeweza kuweka sanamu zao?
msanifu lazima atakuwa ni kijana ambaye alikutana na ile video ya yule chui akikamata mamba kwenye mitandao ya kijamii.. yeye akaona ni bonge la issue bila kufanya research
 
Daah huu ndiyo U great thinker, sijapata huko but this is very valid and good observations. Halafu ni ajabu sana kuweka jaguar wakati Morogoro kuna mbuga za wanyama na nature reserves nyingi tuu, pia milima ya uluguru inayotiririsha maji. Nashauri hii post ukaibandike pia kwenye ukurasa wa Mhe Kigwangala kule Twitter ataufanyia kazi, sometimes yuko sharp.
mlima wanaweka pale round ya masika...
 
Kipindi niko shule ya msingi hapo round about ya msamvu ilikuwa ni mauza mauza tupu,kuna malori yalikuwa yakitoka dar kwenda njia ya dodoma hayataki kuzunguka basi unakuta asubuhi yamegongana,mengine yanapitiliza hapo katikati,mara ya mwisho nilishuhudia lori likitokea dodoma lilipanda huo ukuta unaoanzia hapo njia ya kuingia stendi mpaka mzunguko unapoanzia.

Pia lilikuwa chimbo la vibaka kukatiza na kumaliza vile vinjia kati kati ya ile michongoma bila kula roba ya mbao ilikuwa ni bahati sana.

Siku hizi hali ni shwari kabisa.

Pongezi ziende kwa awamu ya 5 kwa kweli.
 
Back
Top Bottom