Sanamu za wanyama mzunguko (roundabout) wa Msamvu, Morogoro.

Wiki iliyopita nimepita roundabout ya Msamvu na kuona kazi nzuri ya kutengeneza sanamu zinazoonesha vivutio vyetu. Moja ya sanamu hizo ni ile ya chui akimkamata mamba. Nina tatizo na hii sanamu. Jamii ya chui wenye tabia na uwezo wa kukamata mamba wanaitwa jaguars wanaopatikana bara Amerika. Hawa wanafanana kwa muonekano na hawa chui (leopards) tulionao hapa nchini. Na jamii ya mamba ambao huweza kukamatwa/kuliwa na hawa jaguars wanaitwa caimans ambao hupatikana pia bara Amerika. Caimans wanafanana na mamba (crocodiles) hawa tulionao hapa nchini ila wao, pamoja na tofauti zingine, ni wadogo kwa umbile.

Kwa ufahamu wangu hatuna jaguars wala caimans hapa nchini. Kama hivyo ndivyo, nini mantiki ya kuweka sanamu za wanyama ambao hawapatikani hapa nchini wakati tunao wanyama wengi tu ambao tungeweza kuweka sanamu zao?
Exposure ya watu wa local government iko poor sana.,no wonder PM mstaafu mzee pinda aliwahi kuwaponda akasema au kwa sababu mko local govt ndo mnafanya mambo kilocal?
 
Watoe
Period.
Halafu kuna wengine wa.etengeneza twiga ambaye hafanani kabisaa , na kuna nyati hapo kibaha ni kituko kichwa kidogo kama kondoo.
 
Wiki iliyopita nimepita roundabout ya Msamvu na kuona kazi nzuri ya kutengeneza sanamu zinazoonesha vivutio vyetu. Moja ya sanamu hizo ni ile ya chui akimkamata mamba. Nina tatizo na hii sanamu. Jamii ya chui wenye tabia na uwezo wa kukamata mamba wanaitwa jaguars wanaopatikana bara Amerika. Hawa wanafanana kwa muonekano na hawa chui (leopards) tulionao hapa nchini. Na jamii ya mamba ambao huweza kukamatwa/kuliwa na hawa jaguars wanaitwa caimans ambao hupatikana pia bara Amerika. Caimans wanafanana na mamba (crocodiles) hawa tulionao hapa nchini ila wao, pamoja na tofauti zingine, ni wadogo kwa umbile.

Kwa ufahamu wangu hatuna jaguars wala caimans hapa nchini. Kama hivyo ndivyo, nini mantiki ya kuweka sanamu za wanyama ambao hawapatikani hapa nchini wakati tunao wanyama wengi tu ambao tungeweza kuweka sanamu zao?
Mambo ya Morogoro hayo. Mjini kasoro bahari

Sent from my XT1097 using JamiiForums mobile app
 
Wewe ndio wasema hatunao ila wanaotengeneza wanajua kwamba tunao
 
Tuishukuru serikali ya awamu ya tano
Kishindo Cha Awamu Ya Tano

😁😂😅😄😃😃😀😁😂😅😅
Ukiona Mtu Hapendi Amani Ujue Huyo Ni Tatizo Hapa Tanzania
Alikuwa Mkorofi Mpaka Alipokuwa Tumboni Mwa Mama Yake
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Back
Top Bottom