Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimekupata juu ya fumbo hilo. Japo kuna vichwa vibovu vitaendelea kupotosha na kuunishia ukweli halisiSuala la sanduku la agano kwa kweli kwamba limefichwa wapi ni tata,lakini kuna umuhimu na ulazima kwamba tusiwe nalo leo maana kwa kule kufa kwa Yesu msalabani na pazia lililokuwa linapatenganisha patakatifu na patakatifu pa patakatifu(ambapo kimsingi ndipo maskani ya sanduku la agano)kulifanya mwisho wa taratibu za kidini na kwa kuanzia hapo Mungu anakaa ndani yetu na si kwenye maskani maalum tu.
Sasa basi sanduku hilo lingekuwepo hata leo watu wangeshindwa kumwabudu Mungu katika Roho na Kweli na yumkini wengine wangeabudu sanduku hilo.
Nani alienda huko akaliona?original lipo mbinguni hapa duniani kama sample tu copy yake
Kuwa serious basi.Sanduku la agano liko hapa
Ufunuo wa Yohana 11:19
[19]Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi sana.
InawezekanaHaya Mambo yanapasua kichwa Sana inasemakana waliojenga hekalu la kuhifadhi Hilo sanduku walipewa karatasi zenye Mambo ya Siri na mfalme suleiman, wakatokea jamaa wakawavizia na wakawaua hao wajenzi wa hekalu na kuchukua hizo karatasi zenye Siri Sasa Hawa jamaa baada ya kuchukua karatasi za Siri ndio wakaanzisha kitu kinaitwa Freemason upo hapo
Na mimi najua hivyoLipo Ethiopia mpaka leo hii hapa
Wewe ndio umepatia,Mimi nilivyoelewa lipo mbinguni au?
Uko sahihi kabisaHoja ni kwamba sanduku lilikuwa na utukufu wa Mungu na waliokuwa wanaruhusiwa kulishika ni wana wa lawi hakuna mtu mwingine yeyote aliyeruhusiwa kulishika wala kuligusa, aliyethubutu kulishika/kuligusa bila kuruhusiwa alikufa hapohapo.
Je baadae utukufu wa Mungu uliondolewa na kila mtu akaruhusiwa kulishika/kuligusa na kulibeba ndio maana likaweza kubebwa na mtu yeyote asiyekuwa mulawi na kufichwa mahali pasipojulikana pasipokupata madhara yoyote ya kufa kama ilivyokuwa hapo awali?.
Isije ikawa sanduku la Bwana lilifichwa na Mungu mwenyewe kama alivyoificha busitani ya edeni kwa ajili ya usalama wa mwanadamu ili wasiendelee kufa kwa kuwa amri ya Mungu ilikuwa ni wana wa lawi pekee ndio walioruhusiwa kuligusa sanduku la Bwana, tofauti na hapo aliyethubutu kuligusa kama hakuwa mulawi hakuna adhabu nyingine aliopewa zaidi ya kifo.
Na hakuna mahali popote pale tunapoambiwa Kama Mungu alibadilisha amri yake ya kutaka wana wa lawi ndio watu pekee wanaoruhusiwa kuligusa sanduku la Bwana, na kuruhusu kila mtu yeyote aliguse pasipo kupata madhara yoyote.
Wakati wa Sanduku la Agano, sanduku hilo lilikuwa linakaa sehemu inayoitwa Patakatifu pa Patakatifu, sehemu ambayo alikuwa anaruhusiwa kuingia Kuhani tu na kwa mara moja tu kwa mwakaKwa sehemu uko sahihi, lakini hoja yangu iko hapa kama wafilisiti waliweza kulichukua na likaweza kuwaua kwa maana kwamba bado lilikuwa na utukufu wa Mungu na kwamba amri ya kugushwa na wana wa lawi ilikuwa bado inafanya kazi ndio maana liliendelea kuwaua wafilisiti.
Je kwa sasa kama sanduku la Bwana kama bado lipo mahali hapa duniani ile hali ya kufanya makabila mengine kufa kama wataligusa sanduku la Bwana kwa kuwa siyo wana wa lawi iliondolewa ndio maana hatujasikia watu wamekufa kutokana na kugusa sanduku la Bwana? au sanduku la Bwana halipo kabisa hapa duniani ndio maana watu hawafi?.
Uko sahihi, je kipindi Yesu ana zaliwa na kusurubiwa msalabani kuna ushahidi wowote unaothibitisha kuwa Yesu alilikuta?je hilo sanduku ambalo limebaki la kawaida ambalo kwa sasa linaweza likashikwa na kuguswa na mtu yeyote baada ya Yesu kufa kwa sasa liko wapi?.Wakati wa Sanduku la Agano, sanduku hilo lilikuwa linakaa sehemu inayoitwa Patakatifu pa Patakatifu, sehemu ambayo alikuwa anaruhusiwa kuingia Kuhani tu na kwa mara moja tu kwa mwaka
Baada ya Yesu kufa msalabani, pazia lilokuwa linapaficha pataklatif pa patakatifu lilipasuka na hivyo damu ya Yesu kupelekea watu wote wanaomwamini kuwa makuhani (priesthoood of all believers); tukawa sasa chini ya AGANO JPYA, lile la zamani lililokuwa linawakilishwa na SANDUKU LA AGANO, likafutika kuanzia pale
Kwa hiyo kuanzia pale, Sanduku la Agano lilibadilika na kuwa sanduku la kawaida ambalo unaweza uktunzia hata nguo za kuvaa
Issue hapa ipo kabla ya Yesu kufa Msalabani, kwamba Sanduku la Agano liliendelea kuwa ni lile lile kama lilivyowahi kuwa kwenye kipindi kingine chochote cha nyuma kabla ya Yesu kufa msalabani
dhuuuuukuna tetesi ya kuwa hapa Tanzania kwenye misitu ya monduli kuna chombo chenye mfano wa sanduku la agano, ambacho kiliachwa hapo na majeshi ya Ujerumani enzi za ukoloni. Inasemekana kuwa chombo hicho kina miujiza na mambo mengi ya ajabu na kutisha.