Sanduku la Agano liko wapi?

Sanduku la Agano liko wapi?

Alifia mlima Nebo na kuzikwa na Mungu
Baadae alivhukuliwa akapaa mbinguni , Musa yupo hai mbinguni, baadae alimtokea Yesu Wakiwa na nabii eliya ambaye yeye alipaa pia hakuonja kifo ,Musa alionja kifo
 
Suala la sanduku la agano kwa kweli kwamba limefichwa wapi ni tata,lakini kuna umuhimu na ulazima kwamba tusiwe nalo leo maana kwa kule kufa kwa Yesu msalabani na pazia lililokuwa linapatenganisha patakatifu na patakatifu pa patakatifu(ambapo kimsingi ndipo maskani ya sanduku la agano)kulifanya mwisho wa taratibu za kidini na kwa kuanzia hapo Mungu anakaa ndani yetu na si kwenye maskani maalum tu.

Sasa basi sanduku hilo lingekuwepo hata leo watu wangeshindwa kumwabudu Mungu katika Roho na Kweli na yumkini wengine wangeabudu sanduku hilo.
Nimekupata juu ya fumbo hilo. Japo kuna vichwa vibovu vitaendelea kupotosha na kuunishia ukweli halisi
 
Sanduku la agano liko hapa
Ufunuo wa Yohana 11:19
[19]Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi sana.
 
Sanduku la agano liko hapa
Ufunuo wa Yohana 11:19
[19]Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi sana.
Kuwa serious basi.
 
Haya Mambo yanapasua kichwa Sana inasemakana waliojenga hekalu la kuhifadhi Hilo sanduku walipewa karatasi zenye Mambo ya Siri na mfalme suleiman, wakatokea jamaa wakawavizia na wakawaua hao wajenzi wa hekalu na kuchukua hizo karatasi zenye Siri Sasa Hawa jamaa baada ya kuchukua karatasi za Siri ndio wakaanzisha kitu kinaitwa Freemason upo hapo
Inawezekana
 
Hoja ni kwamba sanduku lilikuwa na utukufu wa Mungu na waliokuwa wanaruhusiwa kulishika ni wana wa lawi hakuna mtu mwingine yeyote aliyeruhusiwa kulishika wala kuligusa, aliyethubutu kulishika/kuligusa bila kuruhusiwa alikufa hapohapo.

Je baadae utukufu wa Mungu uliondolewa na kila mtu akaruhusiwa kulishika/kuligusa na kulibeba ndio maana likaweza kubebwa na mtu yeyote asiyekuwa mulawi na kufichwa mahali pasipojulikana pasipokupata madhara yoyote ya kufa kama ilivyokuwa hapo awali?.

Isije ikawa sanduku la Bwana lilifichwa na Mungu mwenyewe kama alivyoificha busitani ya edeni kwa ajili ya usalama wa mwanadamu ili wasiendelee kufa kwa kuwa amri ya Mungu ilikuwa ni wana wa lawi pekee ndio walioruhusiwa kuligusa sanduku la Bwana, tofauti na hapo aliyethubutu kuligusa kama hakuwa mulawi hakuna adhabu nyingine aliopewa zaidi ya kifo.

Na hakuna mahali popote pale tunapoambiwa Kama Mungu alibadilisha amri yake ya kutaka wana wa lawi ndio watu pekee wanaoruhusiwa kuligusa sanduku la Bwana, na kuruhusu kila mtu yeyote aliguse pasipo kupata madhara yoyote.
Uko sahihi kabisa
Kuna kipindi fulani machizi fulani wakati wa vita, waliwahi kulitekaa wakaondoka nalo. Baada ya muda, waliomba wenyewe kulirudisha pasipo kuombwa na mtu

Hili sanduku litakuwa lilifichwa na Mungu; kwa sababu Biblia inathibitisha pia mtu mwingine kuwahi kufa baada ya kulidaka lilipokuwa linataka kuanguka chini, akilizuia lisianguke chini..

Kilichopelekea kifo chake ni kwamba hakuwa wa ukoo ule uliokuwa unaruhusiwa kulishika sanduku hilo, yaani ukoo wa Lawi
 
Kwa sehemu uko sahihi, lakini hoja yangu iko hapa kama wafilisiti waliweza kulichukua na likaweza kuwaua kwa maana kwamba bado lilikuwa na utukufu wa Mungu na kwamba amri ya kugushwa na wana wa lawi ilikuwa bado inafanya kazi ndio maana liliendelea kuwaua wafilisiti.

Je kwa sasa kama sanduku la Bwana kama bado lipo mahali hapa duniani ile hali ya kufanya makabila mengine kufa kama wataligusa sanduku la Bwana kwa kuwa siyo wana wa lawi iliondolewa ndio maana hatujasikia watu wamekufa kutokana na kugusa sanduku la Bwana? au sanduku la Bwana halipo kabisa hapa duniani ndio maana watu hawafi?.
Wakati wa Sanduku la Agano, sanduku hilo lilikuwa linakaa sehemu inayoitwa Patakatifu pa Patakatifu, sehemu ambayo alikuwa anaruhusiwa kuingia Kuhani tu na kwa mara moja tu kwa mwaka

Baada ya Yesu kufa msalabani, pazia lilokuwa linapaficha pataklatif pa patakatifu lilipasuka na hivyo damu ya Yesu kupelekea watu wote wanaomwamini kuwa makuhani (priesthoood of all believers); tukawa sasa chini ya AGANO JPYA, lile la zamani lililokuwa linawakilishwa na SANDUKU LA AGANO, likafutika kuanzia pale

Kwa hiyo kuanzia pale, Sanduku la Agano lilibadilika na kuwa sanduku la kawaida ambalo unaweza uktunzia hata nguo za kuvaa

Issue hapa ipo kabla ya Yesu kufa Msalabani, kwamba Sanduku la Agano liliendelea kuwa ni lile lile kama lilivyowahi kuwa kwenye kipindi kingine chochote cha nyuma kabla ya Yesu kufa msalabani
 
Wakati wa Sanduku la Agano, sanduku hilo lilikuwa linakaa sehemu inayoitwa Patakatifu pa Patakatifu, sehemu ambayo alikuwa anaruhusiwa kuingia Kuhani tu na kwa mara moja tu kwa mwaka

Baada ya Yesu kufa msalabani, pazia lilokuwa linapaficha pataklatif pa patakatifu lilipasuka na hivyo damu ya Yesu kupelekea watu wote wanaomwamini kuwa makuhani (priesthoood of all believers); tukawa sasa chini ya AGANO JPYA, lile la zamani lililokuwa linawakilishwa na SANDUKU LA AGANO, likafutika kuanzia pale

Kwa hiyo kuanzia pale, Sanduku la Agano lilibadilika na kuwa sanduku la kawaida ambalo unaweza uktunzia hata nguo za kuvaa

Issue hapa ipo kabla ya Yesu kufa Msalabani, kwamba Sanduku la Agano liliendelea kuwa ni lile lile kama lilivyowahi kuwa kwenye kipindi kingine chochote cha nyuma kabla ya Yesu kufa msalabani
Uko sahihi, je kipindi Yesu ana zaliwa na kusurubiwa msalabani kuna ushahidi wowote unaothibitisha kuwa Yesu alilikuta?je hilo sanduku ambalo limebaki la kawaida ambalo kwa sasa linaweza likashikwa na kuguswa na mtu yeyote baada ya Yesu kufa kwa sasa liko wapi?.
 
Powers of women. Lipo hapo Ethiopia alikabidhiwa mfalme wa kike wa ithiopia aliyekuwa mrembo kuliko wanawake wote duniani alipomtembelea mfalme Suleiman na kumtunuku pezi la motototo. Jamaa alichanganyikiwa na kumkabidhi mwana mama huyo na KURUDI nalo Ethiopia lipo kwenye Moja ya mahekalu ya zamani
 
Kwa msomi mzuri aliesoma biblia hatakiwi kuuliza lilipo sanduku la agano.Pitia kitabu cha UFUNUO WA YOHANA.Kina majibu ya ni wapi lilipo sanduku la agano.

N.B Katika andiko lako unaposema MUNGU alikuwa juu ya sanduku unakosea Sana.Soma Deuteronomy yote uielewe na uitafakari.Unakumbuka pindi Wafilisti walipolichukua Sanduku la agano wakaenda nalo Gaza kuliwekà ndani ya nyumba ya Mungu wao WA kipagani.Pale patakuonyesha Sanduku lile liliwakilisha nini?
 
Kukusahihisha na pia fuatilia ujue kwamba Yoseph alimtia mimba Maria baada ya kumzaa YESU KRISTO..Lengo la malaika kumtokea Yosefu na kumwambia asimwache Maria Kwa Siri ilikuwa kumlea YESU KRISTO Kwa malezi ya familia kamili yaani Baba na mama.Kwa hii imetuonyesha umuhimu WA Baba ktk familia.

Pili maana ya sanduku la agano ni nini???
Liliwakilisha nini???
Sanduku lilikuwa Kama sanduku lakini lililokuwa limetengenezwa Kwa mazingatio na vipimo vya MUNGU mwenyewe.
AGANO ndio kilichokuwa cha msingi zaidi.Agano ni mkataba WA pande mbili,,au makubaliano ya pande mbili..Kwa hio kisheria kwa leo tungeliita sanduku la mkataba...lilikuwa na fimbo ya haruni iliomeza fimbo za wachawi wa farao.Na haruni alikuwa mlawi..kabila la utumishi wa madhabahu..Mbao zenye amri kumi alizopewa musa nabii alizoandika Mungu mwenyewe..mkate WA mana nk. Kwa Leo hii mkataba e.g WA mwakilishi WA kampuni na bank ama mtu binafsi na benki lazima UWE na maandishi ya makubaliano,,fomu za vigezo wezeshi zenye mashahidi na zilizopitia madaraja kadhaa ya serikali na pia viambatanisho vya rehani..AGANO lile lililokuwa kwenye sanduku ambalo ni mkataba baina ya MUNGU na taifa la Israel alilolichagua lilikuwa halina tofauti na mikataba tulio nayo Leo.Kuna miti miwili ilitumika kulitengeneza sanduku lile,,mlozi na mshita...Kama hua unaisoma biblia vizuri utaona wide range ya matumizi yake pasi na kusahau hisopo..

Kuhusu Maria hawezi fanana na sanduku la agano maana agano jipya lipo katika damu ya YESU KRISTO na damu hio haipo kwenye hekalu la duniani Bali kwenye hekalu lililopo mbinguni..Zaidi kibaolojia mtoto Hana damu ya mama hata chembe,,, Kwa hio baada ya kuchanika pazia la hekalu na utaratibu WA Ibada kubadilika Maria mwenyewe alihitaji kutakaswa na damu yenye thamani kubwa ya YESU KRISTO ili aweze kukikaribia kiti cha rehema.Kwa Sasa kwenye agano jipya utamkiri YESU KRISTO Kama BWANA NA MWOKOZI na Kama njia na uzima then utahesabiwa Haki,,utasamehewa dhambi,,utatiwa mhuri na utakuwa kwenye kundi jipya ama kanisa la Kristo...Na hayo yote anaweza kuyafanya mtu individual pasi na Masada WA mchungaji,,kuhani mkuu ama yoyote mwenye kuwakilisha kwa niaba.
 
Sanduku la agano inasemekana lipo pale Maka chini ya ardhi yake ndipo lilipohifadhiwa tangu kizazi na kizazi. Ndo maana mahala pale ni patakatifu hadi Kesho
 
kuna tetesi ya kuwa hapa Tanzania kwenye misitu ya monduli kuna chombo chenye mfano wa sanduku la agano, ambacho kiliachwa hapo na majeshi ya Ujerumani enzi za ukoloni. Inasemekana kuwa chombo hicho kina miujiza na mambo mengi ya ajabu na kutisha.
dhuuuuu
 
Back
Top Bottom