Sanduku la Agano liko wapi?

Alifia mlima Nebo na kuzikwa na Mungu
Baadae alivhukuliwa akapaa mbinguni , Musa yupo hai mbinguni, baadae alimtokea Yesu Wakiwa na nabii eliya ambaye yeye alipaa pia hakuonja kifo ,Musa alionja kifo
 
Nimekupata juu ya fumbo hilo. Japo kuna vichwa vibovu vitaendelea kupotosha na kuunishia ukweli halisi
 
Sanduku la agano liko hapa
Ufunuo wa Yohana 11:19
[19]Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi sana.
 
Kuwa serious basi.
 
Inawezekana
 
Uko sahihi kabisa
Kuna kipindi fulani machizi fulani wakati wa vita, waliwahi kulitekaa wakaondoka nalo. Baada ya muda, waliomba wenyewe kulirudisha pasipo kuombwa na mtu

Hili sanduku litakuwa lilifichwa na Mungu; kwa sababu Biblia inathibitisha pia mtu mwingine kuwahi kufa baada ya kulidaka lilipokuwa linataka kuanguka chini, akilizuia lisianguke chini..

Kilichopelekea kifo chake ni kwamba hakuwa wa ukoo ule uliokuwa unaruhusiwa kulishika sanduku hilo, yaani ukoo wa Lawi
 
Wakati wa Sanduku la Agano, sanduku hilo lilikuwa linakaa sehemu inayoitwa Patakatifu pa Patakatifu, sehemu ambayo alikuwa anaruhusiwa kuingia Kuhani tu na kwa mara moja tu kwa mwaka

Baada ya Yesu kufa msalabani, pazia lilokuwa linapaficha pataklatif pa patakatifu lilipasuka na hivyo damu ya Yesu kupelekea watu wote wanaomwamini kuwa makuhani (priesthoood of all believers); tukawa sasa chini ya AGANO JPYA, lile la zamani lililokuwa linawakilishwa na SANDUKU LA AGANO, likafutika kuanzia pale

Kwa hiyo kuanzia pale, Sanduku la Agano lilibadilika na kuwa sanduku la kawaida ambalo unaweza uktunzia hata nguo za kuvaa

Issue hapa ipo kabla ya Yesu kufa Msalabani, kwamba Sanduku la Agano liliendelea kuwa ni lile lile kama lilivyowahi kuwa kwenye kipindi kingine chochote cha nyuma kabla ya Yesu kufa msalabani
 
Uko sahihi, je kipindi Yesu ana zaliwa na kusurubiwa msalabani kuna ushahidi wowote unaothibitisha kuwa Yesu alilikuta?je hilo sanduku ambalo limebaki la kawaida ambalo kwa sasa linaweza likashikwa na kuguswa na mtu yeyote baada ya Yesu kufa kwa sasa liko wapi?.
 
Powers of women. Lipo hapo Ethiopia alikabidhiwa mfalme wa kike wa ithiopia aliyekuwa mrembo kuliko wanawake wote duniani alipomtembelea mfalme Suleiman na kumtunuku pezi la motototo. Jamaa alichanganyikiwa na kumkabidhi mwana mama huyo na KURUDI nalo Ethiopia lipo kwenye Moja ya mahekalu ya zamani
 
Kwa msomi mzuri aliesoma biblia hatakiwi kuuliza lilipo sanduku la agano.Pitia kitabu cha UFUNUO WA YOHANA.Kina majibu ya ni wapi lilipo sanduku la agano.

N.B Katika andiko lako unaposema MUNGU alikuwa juu ya sanduku unakosea Sana.Soma Deuteronomy yote uielewe na uitafakari.Unakumbuka pindi Wafilisti walipolichukua Sanduku la agano wakaenda nalo Gaza kuliwekà ndani ya nyumba ya Mungu wao WA kipagani.Pale patakuonyesha Sanduku lile liliwakilisha nini?
 
Kukusahihisha na pia fuatilia ujue kwamba Yoseph alimtia mimba Maria baada ya kumzaa YESU KRISTO..Lengo la malaika kumtokea Yosefu na kumwambia asimwache Maria Kwa Siri ilikuwa kumlea YESU KRISTO Kwa malezi ya familia kamili yaani Baba na mama.Kwa hii imetuonyesha umuhimu WA Baba ktk familia.

Pili maana ya sanduku la agano ni nini???
Liliwakilisha nini???
Sanduku lilikuwa Kama sanduku lakini lililokuwa limetengenezwa Kwa mazingatio na vipimo vya MUNGU mwenyewe.
AGANO ndio kilichokuwa cha msingi zaidi.Agano ni mkataba WA pande mbili,,au makubaliano ya pande mbili..Kwa hio kisheria kwa leo tungeliita sanduku la mkataba...lilikuwa na fimbo ya haruni iliomeza fimbo za wachawi wa farao.Na haruni alikuwa mlawi..kabila la utumishi wa madhabahu..Mbao zenye amri kumi alizopewa musa nabii alizoandika Mungu mwenyewe..mkate WA mana nk. Kwa Leo hii mkataba e.g WA mwakilishi WA kampuni na bank ama mtu binafsi na benki lazima UWE na maandishi ya makubaliano,,fomu za vigezo wezeshi zenye mashahidi na zilizopitia madaraja kadhaa ya serikali na pia viambatanisho vya rehani..AGANO lile lililokuwa kwenye sanduku ambalo ni mkataba baina ya MUNGU na taifa la Israel alilolichagua lilikuwa halina tofauti na mikataba tulio nayo Leo.Kuna miti miwili ilitumika kulitengeneza sanduku lile,,mlozi na mshita...Kama hua unaisoma biblia vizuri utaona wide range ya matumizi yake pasi na kusahau hisopo..

Kuhusu Maria hawezi fanana na sanduku la agano maana agano jipya lipo katika damu ya YESU KRISTO na damu hio haipo kwenye hekalu la duniani Bali kwenye hekalu lililopo mbinguni..Zaidi kibaolojia mtoto Hana damu ya mama hata chembe,,, Kwa hio baada ya kuchanika pazia la hekalu na utaratibu WA Ibada kubadilika Maria mwenyewe alihitaji kutakaswa na damu yenye thamani kubwa ya YESU KRISTO ili aweze kukikaribia kiti cha rehema.Kwa Sasa kwenye agano jipya utamkiri YESU KRISTO Kama BWANA NA MWOKOZI na Kama njia na uzima then utahesabiwa Haki,,utasamehewa dhambi,,utatiwa mhuri na utakuwa kwenye kundi jipya ama kanisa la Kristo...Na hayo yote anaweza kuyafanya mtu individual pasi na Masada WA mchungaji,,kuhani mkuu ama yoyote mwenye kuwakilisha kwa niaba.
 
Sanduku la agano inasemekana lipo pale Maka chini ya ardhi yake ndipo lilipohifadhiwa tangu kizazi na kizazi. Ndo maana mahala pale ni patakatifu hadi Kesho
 
kuna tetesi ya kuwa hapa Tanzania kwenye misitu ya monduli kuna chombo chenye mfano wa sanduku la agano, ambacho kiliachwa hapo na majeshi ya Ujerumani enzi za ukoloni. Inasemekana kuwa chombo hicho kina miujiza na mambo mengi ya ajabu na kutisha.
dhuuuuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…