Sandwich ya mayai ya kukaanga

farkhina

Platinum Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
14,568
Reaction score
16,917
Hii ni 30 minutes or less breakfast, ila unaweza kula mda upendao au hata kuweka kwenye lunchbox ukabeba kazini.


Mahitaji( kwa ajili ya sandwich 4)


1)Slesi 4 za mkate

2)Majani ya kotmir (giligilani) kiasi, unaweza kuweka iliyosagwa pia

3)Kitunguu saumu 1/4 kijiko cha chai

4)Bizari ya manjano kidogo sana

5)Blueband 1/2 teaspoon kwa ajili ya kupakaa kwenye slices zetu za mkate.

6)Pilipili mboga, kata ndogo ndogo unaweza weka na pilipili ya kuwasha ukipenda.

7)Chumvi kiasi.

8)Mayai 3 ukubwa kiasi.

9)Kitunguu maji 1/2.

Namna ya kutaarisha mayai kwa ajili ya sandwich

Weka mafuta kidogo kwenye pan

Kaanga kitunguu maji kwa dakika 2 alafu weka pilipili mboga

Weka saumu,bizari,chumvi na giligali kaanga kwa muda mfupi.

Kabla viitunguu havijawa brown weka mayai na koroga yachanganyike na vitunguu na kuwa vipande vipande, alafu weka katika bakuli yapoe.

Namna ya kutaarisha sandwich

Pakaa blueband kwenye slices zako za mkate na weka mayai kama ufanyavyo kwa sandwich za kawaida....

Weka kwenye jiko la sandwich.

Tazama kama tayari kuiva.

Toa tayar kwa kuliwa.
 
Eti mumie kama sina jiko la sandwich naweza kutumia ujanja gani mwingine?
 
Nzuri ila mie na mayai hapana.
 
Dada hiyo rangi nyeusi ya kwenye mkate imepatikana vipi? Na je? kuna aina nyengine ya sandwich zaidi ya hii.
Nalog off
 
farkhina hiyo sandwich maker ndo inayotoast kabisa mikate au unatoast kabla??
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…