Duh Umenipeleka mbali sana. Sijui kwa nini nimekumbuka hizi nyimbo mbili Embakasi - Les Mangelepa na Carl Douglas - Kung fu fighting
"... iiii nakolele zaina eee x2
Zaina mobali na bandeko ya motema eee, ooo mamaaa"...
Da nimekumbuka enzi za kufichiwa "sindano"
Lakini vivyo hivyo nilicheza santuri japo kwa sauti ya 'kuisikilizia'
Watanielewa wakongwe tu.
mkuu kufichiwa sindano kivipi
"... iiii nakolele zaina eee x2
Zaina mobali na bandeko ya motema eee, ooo mamaaa"...
Da nimekumbuka enzi za kufichiwa "sindano"
Lakini vivyo hivyo nilicheza santuri japo kwa sauti ya 'kuisikilizia'
Watanielewa wakongwe tu.
'Baba zetu' walikuwa watunzaji sana wa vitu vyao, iwe redio, kurunzi, gobole nk...
Shelfu za vitabu utafikiri askari wa Hitla!
Hawakutuamini sana 'watoto' wao (japo tungeweza kuaminika)
'Sindano' ni pin fulani inayogusa santuri inapozunguka na kutoa sauti muafaka...
Walikuwa wanadhani tutaharibu 'player' zao wasipo itoa nakuficha ili tusifungulie (tusicheze) santuri.
Tena kama ni chenja (changer) ndiyo kabisaaa!
Hahahaaa mpwa umri umesonga bhana japo kasura ni kabebiface
Niliutendea haki ujana wangu mpwa
Kiongozi,afro hainyolewi bali inafugwa!aisee naona aisee
enzi zako zile umenyoa na afro lako
Ngazi ngapi kiongozi.Hahahahaaaa raizon pia ninazo
Umenirudisha mbali tena kwa neno DINGI. Je asili yake ni vipi? Sie tulikuwa na senior brother tunamwita mpaka sasa (between ourselves) dingi mdogo ingawa wote tuko mababu tiyari. Alikuwa hodari sana kwa makwenzi. Na mpaka sasa hajui kuwa dingi mdogo ni yeye. Or may be he knows?Duu mpaka nimesisimka kweli kabisa dingi akiondoka anaficha sindano!(laser ya siku hizi) unabaki na limashine tuu