Sarafu ya Iran yashuka hadi chini kabisa huku kukiwa na mvutano kati yake na Marekani na Ulaya

Sarafu ya Iran yashuka hadi chini kabisa huku kukiwa na mvutano kati yake na Marekani na Ulaya

Sarafu ya Iran yashuka hadi chini kabisa huku kukiwa na mvutano kati yake na Marekani na Ulaya.

Sarafu ya Iran iliendelea kuporomoka siku ya Jumamosi, na kudorora zaidi dhidi ya dola ya Marekani huku kukiwa na sintofahamu kuhusu kukaribia kwa Donald Trump katika Ikulu ya White House na mivutano na nchi za Magharibi kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran.

Sarafu ya Iran maarufu kama (Rial), ilishuka hadi 756,000 kwa dola moja kwenye soko lisilo rasmi siku ya Jumamosi, ikilinganishwa na Rial 741,500 siku ya Ijumaa, kulingana na Bonbast.com, ambayo inaripoti viwango vya ubadilishanaji. Tovuti ya bazar360.com ilisema dola hiyo moja ilikuwa ikiuzwa kwa takriban Rial 755,000.

Uchumi hauna siasa ukiona mtu anafanya drama za uchumi na siasa mwangalie alafu cheka. Hujasikia jamaa wa kwa chra walishusha dola dhidi ya tz na sasa wanaenda kuipandisha mpaka mshangae?
 
Muongo mmoja mnaleta mambo kwa mihemko kama ww analyses je irani ni maskini kuliko bongo au jee leo ndio mwanzo wa vikwazo au umejia leo irani yupo under critical embargo ukishakujua hayo hata hiki usingekiandika maana kama 40 yrs and above inakuaje unashtuka mda huu kama hela yake imeshuka mbona yupo hv miaka yote je ilipanda against who??
Pole ndugu. Punguza hasira, toa elimu. Makasiriko yatakuzeesha mapema.
 
Ww kigagura wa ccm una nini cha kuwashauli wairan?
Kwani tangu sh ianze kupanda dhidi ya dora ni kipi kilicho badilika kwenye maisha ya kila siku ya Mtz?
Thamani ya fedha kushuka dhidi ya sarafu za kigeni hakuna mahusiano yeyote na kushuka kwa uchumi bali huwa inashababisha mfumko wa bei hasa iwapo nchi hiyo itakuwa tegemezi wa bidhaa kutoka nje.

Kupanda kwa dora hakuwaathiri moja kwa moja raia waliko ndani ya Iran kwa sababu bidhaa nyingi wanazo tumia ndani ya nchi hiyo zinatokana na viwanda vyao wenyewe na bidhaa zinazo toka nje kwa wingi hasa chakula serikali inazilipia ruzuku , usidhani Iran ni kama nchi yako ambayo mpaka chupi inategemea kuagiza china.

Pia Iran haina madeni kwenye mabenki ya kimagharibi ambayo ingehitaji dora kuyalipa.

Ila hii itawaimiza wairan wenyewe uraia pacha ambao wana safiri safiri sana.

Pesa ya Zambia ina thamani mara tano ya pesa ya S.korea na Japan sasa niambie zambia ina nini za cha maana zaidi ya njaa na umasikini?

Hela ya Iran haina thamani ila raia wa Iran hawajui mgao wa umeme,maji ,wana elimu bora,miundo mbinu ya kisasa,wana sekta kubwa ya viwanda ,wana sekta bora ya afya.

Wakati Tz ambayo fedha yake ina thamani mara 10 ya Iran lakini haina hata kipaumbele chochote kama taifa inajiendea tu kama gari bovu.

Kwahiyo dollar ikipanda watu wasilalamike wala kuitukana serikali maana haina tija?

NB: ni dollar sio dora.
 
Sarafu ya Iran yashuka hadi chini kabisa huku kukiwa na mvutano kati yake na Marekani na Ulaya.

Sarafu ya Iran iliendelea kuporomoka siku ya Jumamosi, na kudorora zaidi dhidi ya dola ya Marekani huku kukiwa na sintofahamu kuhusu kukaribia kwa Donald Trump katika Ikulu ya White House na mivutano na nchi za Magharibi kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran.

Sarafu ya Iran maarufu kama (Rial), ilishuka hadi 756,000 kwa dola moja kwenye soko lisilo rasmi siku ya Jumamosi, ikilinganishwa na Rial 741,500 siku ya Ijumaa, kulingana na Bonbast.com, ambayo inaripoti viwango vya ubadilishanaji. Tovuti ya bazar360.com ilisema dola hiyo moja ilikuwa ikiuzwa kwa takriban Rial 755,000.

View: https://x.com/TheHarrisSultan/status/1869892312836518291
 
Back
Top Bottom