Sarah Baartman: Mwanamke mweusi kutoka Afrika Kusini aliyesafirishwa Ulaya kwa maonesho ya makalio makubwa

Vera sidika



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sijui hiyo Phd ameipata mwaka gani, nachojua kwenye Makala zake alikuwa anaandika tu "Na Sabatho Nyamsenda" huko ndiko nilikomjulia mkuu.

Inawezekana, kuna vile unafanya PHD Makerere kama ilivyoandikwa hapo lakini ukiwa Dar.

Maana dogo kipindi hicho 2012 yote nilikuwa nakaa naye jirani akiwa either Assistant Lecturer/Tutorial, sikumbuki vizuri.
 
Hakika umenifundisha jinsi msomi anavyo paswa kuandika..

Heko kwa makala bora kabisa yenye mifano inayoendana na hadhara.
 
Yaani nimesoma kwa taabu sana mpaka nimefika mwisho ni kwa neema tu 😂
 
izo gazeti peleka Sani na Ijumaa uko
 
Sara Baartman alikuwa ni mwanamke mwenye makalio makubwa yalioshangaza ulimwengu kiasi cha kutumika kwenye maonyesho huko Ulaya. Pia mashavu ya uke(labia) wake yalikuwa marefu kwa kuwa ni tamaduni ya kabila lao, kitu ambacho siku hizi kinaonekana kama ni Female Genital Mutilation

Sara Baartman alizaliwa 1789 katika jamii ya kifugai ya Khoisan, alikulia kwenye mashamba ya kikoloni. Sara aliuzwa kwa kaburu piter willem ambaye alimpeka Cape town, na wakamuita Saartjie jina la kikaburu lenye maana sawa na Sara

Aliingia mkataba octoba 29, 1810 na dkt. William Dunlop, masharti ya kiwa kukubali kusafiri na dkt huyo kuwa mtumishi wake wa ndani na pia kutumika katika maonyesho na burudani. Ilikubaliwa kupata pesa kidogo katika maingizo ya fedha hizo ili arejee afrika kusini baada ya miaka mitano, swala la kusaini mkataba huo ni kizungumkuti kwa kuwa sara hakuwa anajua kusoma na kuandika.

Umbo la sara lililokuwa na makalio makubwa liliwashangaza wazungu ambao walikuwa wanajiona bora. Watu wakawa wanalipa kumuona sara akiwa uchi, kuyaangalia makalio yake na uke wake uliokuwa umerefushwa mashavu yake (Labia) kwa tamaduni za kabila lake

Stember 1814 awalienda ufaransa na akauzwa kwa mfanyabiashara Reaux, na akaendelea kutumika kwenye maonyesho huko Paris

March 1815 akachukuliwa kama kielelezo cha kisayansi, science specimen akitumika na wana anatomia, zoolojia, fiziolojia

Sara alikuwa akiwa na umri wa miaka 26, waliukata mwili wake na kuuweka katika makumbusho hadi mwa 1974, hadith ya sara ilifufuka mwaka 1981 Stephen Jay Gould alipoanza kuipinga sayansi ya kibaguzi.

Serikali ya Nelson mandela iliposhinda kupitia chama cha ANC ilianza mazungumzo na serikali ya ufaransa ili kuurudisha mabaki ya mwili wa Sara. Hatua hiyo ilichukua miaka nane, machi 6 2002, mwili wake ulirudishwa afrika kusini na akazikwa agosti 9, 2002.

 
Katika miaka 1789-1815 palikuwepo na wanawake wawili wenye makalio makubwa, mmoja wapo aliitwa Sarah Baartman mwenye kutokea kabira la Khoi Khoi NCHINI Afrika Kusini. Wakoroni walivutiwa nae na kumchukua kwenye makumbusho NCHINI Ufaransa akitumika Kama kivutio. Kwa miaka hiyo biashara ya Human Zoo ilikuwa imetawala. Binadamu walikuwa wakiwekwa kwenye maonyesho Kama inavyofanyika kwa wanyama (animal zoo).

Sarah Baartman alifariki akiwa na miaka 29 mwaka 1815, hata alipofariki mwili wake uliwekwa makumbusho kwa malengo ya kisayanyasi atumike Kama specie sample ya kujifunzia. Hadi ilipofikia mwaka 1970 pale Muafrika Kusini aliyefahamika kwa jina Diana, aliandika shairi la kumhusu Sarah Baartman lenye tungo moja ikisisema "...nimekuja Kuirudisha nyumbani..." Utunzi wa shairi hili ukazua gumzo duniani na ukapata kasi zaidi mwaka 1980 lilipotungwa shairi lingine juu yake.

Mnamo 1994 baada Afrika Kusini kupata Uhuru wa kujitawala, Nelson Mandela aliomba kupitia serikali ya Ufaransa kuomba mabaki ya Sarah Baartman yarudi Afrika Kusini na yapate kuzikwa. Hadi mwaka 2002 masalia hayo yakarudi na kuzikwa na kufanyiwa sehemu ya maonyesho ya kihistoria.



Mfahamu Pia Sarah Baartman aliweza kupewa majina mbali mbali Kama vile Venus n.k
 
unafahamu maana ya ya Female Genital Mutilation? I am not sure kama unafahamu.



 
Alijulikana Kama Sarah Baartman

.

Inadhaniwa kuwa alizaliwa katika jimbo la Afrika Kusini la Eastern Cape mwaka 1789, mama yake alifariki dunia alipokuwa na umri wa miaka miwili na baba yake, mfugaji, alifariki alipokuwa katika umri wa kubalehe.

Aliingia katika utoaji wa huduma za nyumbani mjini Cape Town baada ya mkoloni Mholanzi kumuua mwenza wake, ambaye alikuwa tayari amezaa naye mtoto ambaye alikufa

Aliletwa Ulaya kwa njia za madai ya uongo na daktari Muingereza , akiitwa kwa jina la jukwani "Hottentot Venus", ambapo alioneshwa katika kumbi za "maonyesho ya vituko" mbali mbali katika miji ya London na Paris, huku umati wa watu ukialikwa kuyaangalia makalio yake makubwa.

Haya yalimfanya asababishe mvuto wakati alipokuwa akifanya onyesho katika eneo la Piccadilly Circus jijini London baada ya kuwasil

Jukwaani alivaa nguo ya kubana mwili wake ( skin-tight) yenye rangi, pamoja na shanga na manyoya na alikuwa akivuta tumbaku. Wateja matajiri walikuwa wanalipa pesa zao kwa ajili ya kuburudishwa kibinafsi majumbani mwao, huku wageni wakiruhusiwa kumgusa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…