Sare mpya Kwa madereva bodaboda DAR

Sare mpya Kwa madereva bodaboda DAR

Hilo joto na hizo sare mtawaumiza tu boda boda, ni bora mbunifu angepunguza akafanya simple kama mfumo wa mikanda ya viakisi mwanga (reflector)
 
Wivu wao tu..wakiona boda boda wanapiga hesabu za maokoto vzr wanataka na wao wachukue humo humo
Wewe jiulize sare mpya picha ya raisi inahusikaje hapo, na kitambulisho picha ya raisi inahusikje tena hapo.

Wajenge barabara bora magari yanayoenda yasiingiliane na yanayotudi uwone kama kuna ajali....

Hili la vitambulisho ni mradi mpya wa kodi wameubuni
 
Kila siku wanashindwa kukusanya kodi, tatizo sio sare kama ni ajali. Wekeza kwenye barabara bora uwone kama ajali utasikia....
Mkuu hizi ni sababu kuu 3 za ajali za barabani.

1. Miundombinu ya barabara
2. Uzembe wa madereva
3. Ubovu wa vyombo vya usafiri.

Kwahiyo hata ikitokea ukaweka miundombinu mizuri ya barabara bado hizo sababu nyingine zitakuangusha
 
Wewe jiulize sare mpya picha ya raisi inahusikaje hapo, na kitambulisho picha ya raisi inahusikje tena hapo.

Wajenge barabara bora magari yanayoenda yasiingiliane na yanayotudi uwone kama kuna ajali....

Hili la vitambulisho ni mradi mpya wa kodi wameubuni
Wanahisi hiyo picha italeta ushawishi kwa wahusika na kujiunga wengi lkn pia ni mileage ya mwenye picha...lkn pia ni faida kwa aliyesema iwekwe maana amejua kucheza na fursa
 
Sare mpya kwa Madereva Bodaboda Dar es salaam

Hivi karibuni zitazinduliwa sare mpya kwa madereva wa Bodaboda Dar es salaam ambapo sare hizo zitakuwa na namba na ukiingiza hiyo namba kwenye mfumo utajua taarifa zote za huyo dereva na sehemu anapotokea.
Ambapo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Muheshimiwa Edward Mpogolo, akiwa ametinga uniform Maalum ya madereva bodaboda ambayo inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni jijini Dar es salaam. Hii nzuri sana itasaidia kupunguza vitendo vya wizi na kwa madereva hao kwani baadhi yao sio waaminifu na kuhamasisha usafi.Tunapoelekea dereva wa Bodaboda akifanya lolote lile ambalo sio zuri inakuwa rahisi kumpata.
Hii nzuri sana isiishie Dar es salaam iwe kwa bodaboda Tanzania nzima

Wale bodaboda ambao wanakimbia baada ya kusababisha ajali au wale ambao wanavunja side mirror na kukimbia hapa itakuwa mwisho waoView attachment 2949037.
Iwe kwa Tanzania nzima na iwe lazma
 
Sasa kwanini iwekwe picha ya samia badala ya dereva
 
Mimi naona ni uniform za kampeni tu hapa na picha kuwa hakuna mwingine
Mavazi ya boda lazima yawe magumu sana kumsaidia asivunjike na ni ghali mno
Sasa hivyo vitambaa vinasaidia nini?
Usalama kwanza
 
huo ni mradi wq manispaa wakuwapiga maokoto maafsa usafirishaji ,
suala uchawa pia lishaota mizizi sana kumshirikisha muheshimiwa rais katika petty issues kunaondoa heshima ya hio title ataonekana kama mapedeshee tu wanaopenda kusifiwa ili wamwage manoti
Hahahah papah musofeee
Mamah ashah baraka na kati ya twanga pepetaah
Piga kelele kwa mamahh akee
 
Kwanza natoa shukrani kwa mama kwa kuniwezesha kukopa bundle na kuweza kuingia JF.

Pili, kuhusu picha ya mama, ipo hapo kama motisha kwa kijana wa bodaboda kujituma kwa ari na nguvu zote ili awe kama mama😀😀😀😀.

Wamesahau hijab tu ndani ya helmet.
🤣🤣🤣Waongezeh hijab tubalance
 
Wanahisi hiyo picha italeta ushawishi kwa wahusika na kujiunga wengi lkn pia ni mileage ya mwenye picha...lkn pia ni faida kwa aliyesema iwekwe maana amejua kucheza na fursa
Tatizo bongo tulionalo wale wenye uwezo mkubwa ndio wako mtaani wanatafuta ajira, wale wenye uwezo mdogo ndio hao wako serikalini.

Hivi raisi hawezi akahoji kwanini picha yangu imewekwa hapo kwenye jezi? Au ndio mwendelezo wa aliyeanzisha
 
Mkuu hizi ni sababu kuu 3 za ajali za barabani.

1. Miundombinu ya barabara
2. Uzembe wa madereva
3. Ubovu wa vyombo vya usafiri.

Kwahiyo hata ikitokea ukaweka miundombinu mizuri ya barabara bado hizo sababu nyingine zitakuangusha
Kila nchi ina wazembe, ubovu wa magari unachagizwa na barabara, tuwe na barabara nzuri alafu tuache au tupunguze kuagiza gari used
 
Ni upigaji huu Kama upigaji mwingine. Waambie walete nguo ama sare ama wasajiliwe wapewe namba bure hizo sare za Nini na huku boda Ina plate number white ,unamlazimisha mtu kushindia nguo moja tu
 
Back
Top Bottom