Leonel Ateba Mbinda
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 644
- 2,695
Jana nilicheki mechi baina ya Real Mallorca vs Real Madrid, gemu iliisha kwa sare ya bao 1 -1, mpira mwingi ulipigwa na Real Mallorca jana na almanusura Madrid walie dakika za mwisho, Real Madrid ndio mabingwa wa soka duniani, ndio timu yenye mafanikio makubwa namba duniani, timu yenye makombe yasiyohesabika duniani.
Madrid imesheheni wachezaji wa hatari kabisa, kule mbele kuna watu wabaya mno.Jana Vini, Mbappe, Rodrigo walihangaika mnooo lakini wapi, Mallorca walipambana nao bila kujali majina.
Lakini kubwa zaidi na hoja yangu mimi ni Madrid kusare na timu ndogo kama Mallorca, sare ya jana haikuwashtua mashabiki wala kocha wala uongozi, sare katika mchezo wa kwanza ni jambo la kawaida hasa ukizingatia kuwa ndio kwanza mechi ya kwanza kwao.
Lakini pia wenzetu wanaamini sare ni sehemu ya mchezo, Madrid wamepambana sana lakini matokeo yakawa vile vile moja moja, walishambulia sana lango la Mallorca na Mallorca hawakuwa wanyonge kivile, waliwapelekea moto Madrid mwanzo mwisho.Huo ndio mpira.
Kwenu mashabiki wa Simba, timu yetu inapotoka sare au kufungwa ni sehemu ya mchezo, nafikiria jana Simba angesare au kufungwa sijui ingekuwaje leo Jumatatu, kama wewe unaona football iko upande wa ushindi tafadhali geuka kama Hamissa Mobetto au Meja Kunta au Nabii Meja nenda Yanga ambao wao wanaamini kushinda kila gemu ndio mpango mzima.
Kama Madrid anatoka sare na kibonde wewe nani uwe unashinda kila siku.