ankai
JF-Expert Member
- Nov 25, 2017
- 3,282
- 4,251
Mkazi wa morogoro Abubakari Mbaya (22) anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani pwani kwa tuhuma za kukutwa amevaa sare z jeshi la wananchi Tanzania JWTZ wakati yeye akiwa si askari wa jeshi ilo.
Kijana huyo alikamatwa juzi jioni na askari halisi baada ya kutiliwa shaka eneo la kwa Mathiasi mjini Kibaha.
Kamanda wa polisi mkoa wa pwani Wankyo Nyige alisema kijana uyo alikuwa anasafiri na basi la Abood kutoka Morogoro kuelekea Dar esalaam akiwa amevalia sare izo za jeshi.
Kwa mujibu wa kamanda kijana baada ya kukamatwa alikiri kuwa kuwa ni kweli yeye si askari wa jeshi la wananchi na pia izo sare alizokuwa amevaa ni za babu yake ambaye alikuwa ni askari wa jeshi lakini kwa sasa ameahafariki .
Kijana aliweka wazi kuwa amekuwa akivaa sare izo za jeshi kutokana na mapenzi makubwa sana aliyonayo juu ya kazi iyo ya kulitumikia taifa kupitia jeshi la wananchi lakini amejaribu kila mbinu angalau aweze kupata nafasi ya kulitumikia jeshi ilo lakini kwake imekuwa ngumu sana.
Aliongeza kuwa tangia akiwa mdogo enzi za babu yake akiwa hai amekuwa akivaa izo umsare na muda mwingine alikuwa akimwibia babu yake.
Kijana hakusita kufikisha kilio chake kwa Mh Raisi waTanzania kwamba anamuomba kama itampendeza basi ampe nafasi ya kujiunga na jeshi la wananchi kwani anapenda kulitumikia taifa kwa moyo mmoja na ni kazi ya ndoto zake ambayo amekuwa akiiota siku zote za maisha yake.
Hata Kamanda alisema baada ya kijana kuhojiwa na uchunguzi kukamilika atafikishwa mahakamani ili akajibu tuhuma zinazo mkabili za kutumia sare za chombo cha ulinzi ili hali yeye si muhusika.
Maoni yangu kamanda haoni kama uyu kijana ni mzalendo wa hali ya juu kwa taifa lake kwanini wasimsaidie kukamilisha ndoto zake ili aje kuwa mtumishi mwenye kuipenda na uzalendo uliotukuka juu ya nchi yake kuliko kumfikisha mahakamani ili akafungwe?