Sare za JWTZ zamuweka kijana matatani

Sare za JWTZ zamuweka kijana matatani

Sheria ni sheria tu. Apewe adhabu yake kisha kama kuna namna asaidiwe ajiunge na jeshi
 
Kuna video ya huyu kijana mbona nitukio la siku nyingi hili
Kuwa tukio la siku nyingi kuna husiana vip hiii mada inayojadiliwa apa ndani mkuu au likisha kuwa ni tukio la siku nyingi halitakiwi tena kujadiliwa?
 
ingekua nchi za wenzetu wangeangalia uwezekano wa kumuingiza jeshi,kwa maana anaonesha anaitamani sana kazi hiyo,lakini hapa kwetu anabahati sana kukamatwa na jeshi la polisi ,saa hizi angeshakuwa uji.
And there is where the difference btn 1st world anf 3rd world come from !
 
Asitafute huruma!
Mara nyingi askari akifariki au hata kustaafu au kuacha kazi kwa utaratibu vifaa vyake vyote vya kijeshi vinarudishwa jeshini.
Aseme vizuri hizo nguo alikuwa anazifanyia kazi gani?!
😡😡😡😡😡😡😡😡😡
Unaa huo.
 
Wajinga sana hawa vijana majeshi yote...sheria kuu ni usafi usafi usafi....kuanzia mwili hadi mavazi kinacho sababisha wanashukiwa kuwa si wanajeshi ni kutokana na 1.kuchanganya sare na mavazi mengine ambayo hayaendani
2.mtu anashindwa kuzipunguza ziendane na umri wake...
3.sare kubwa kama mfuko wa kutolea unga kwenye mashine ya kusaga.
4.unyoaji wa kiaskari unajurikana
5.kutokuvaa sare zilizokamilika kuanzia kofia hadi buti.
6.kutokujua tabia za kiaskari

Hapo lazima ukamatwe tu
Haaaaaa kwelii mkuu, vijana wengi hawajui tabia na mwenendo wa askari au mwanajeshi
Nywele ndefu. Ndevu hajanyoa, sare gwanda inapgwa mixer na li t shirt rangi cyo hapo lazima tu uingie kumi na nane
 
Askari muda wote anatakiwa kuwa timirifu...kama yupo na un-form....
Sasa awa askari feki
Utakuta kavaa
1.gwanda na Raba
2.Kavaa gwanda lakini hajavaa kofia.
3.kavaa kofia na gwanda lakini kofia kavaa anavyojua yeye wakati kofia inauvaaji wake kuna baret na cape kila moja inavaliwa kwenye mission maalum.
4.salamu za kijeshi/kiaskari hapo sasa ndipi wengi wanapo uvaa mkenge na kujikuta mapema wanakamatwa
Haaaaa kweli wengne hata mkanda anakosea kuuvaa!!
 
Kama huna nia mbaya utayavaa mavazi hayo kwa sababu ni ya kufanyia mazoezi au?? Mambo mengine ni ujuha tu unawasumbua watu. Anayeyavaa bila halali nia yake awapate wajinga awaibie
 
Yanaingiaje?
Yanapita wapi?
Yanauzwa wapi?
Why mnadili na wanunuzi na sio wauzaji?
Maswali ni mengi kuliko majibu!

Kingine mie huwa nawashangaa wanaoyavaa coz sionagi hata mvuto wake!
 
Back
Top Bottom