liwaya
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 2,384
- 1,648
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
sisi Simba tumeshinda 1 kwa bila
Michezo mitatu ya Kigi kuu.View attachment 1704933
Michezo mitatu ya Kigi Kuu ya Soka Tanzania Bara imechezwa hii leo katika viwanja tofauti
Baada ya kuondoka na alama 1 katika mchezo dhidi ya Mbeya City juma lililopita, Yanga hii leo wameambulia alama moja pia baada ya mchezo wake dhidi ya Kagera Sugar kumalizika kwa sare ya 3-3
Magoli ya Yanga yamefungwa T. Kisinda 14', D. Kaseke 30' na M. Tonombe 61' huku magoli ya Kagera Sugar yakifungwa na P. Mwalyanzi 11', H. Mwaterema 24' na Y. Mhilu 45'+2
Mchezo huo umehusisha magoli mengi zaidi kuliko michezo mingine iliyopigwa hii leo
Aidha, baada ya kumlazimisha Azam kichapo cha goli 2-1 katika Dimba la Mkwakwani, Coastal Union hii leo wamerejeshewa adhabu ya goli 2-1 na Dodoma Jiji katika Dimba la Jamhuri huko Dodoma
Magoli ya Dodoma Jiji yamefungwa na A Jabir 57' na J Mtegeta 66' , huku goli la Wagosi wa Kaya likifungwa na R Hafidh 83'
Mchezo mwingine uliopigwa hii ni leo ni kati ya Mtibwa Sugar ambao walikuwa nyumbani kwenye uwanja wa Jamhuri kuumana na Ihefu FC. Si Mtibwa wala Ihefu ambaye alionyesha ubabe wake baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 1-1
Goli la Mtibwa limefungwa na K Sabato kunako dakika ya 38, huku goli la Ihefu likifungwa na I Ngoah dakika ya 13